Arusha
Home » » PATA PICHA ZAIDI ZA RAIS KIKWETE AKIKABIDHI NG’OMBE 500 NGORONGORO.

PATA PICHA ZAIDI ZA RAIS KIKWETE AKIKABIDHI NG’OMBE 500 NGORONGORO.

 Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, akizungumza na wakazi wa Kitongoji cha Waso wilayani Ngorongoro.
 Ng'ombe waliotolewa na Rais Kikwete
 
Genereta za kuzalisha umeme katika kituo cha umeme cha Ngorongoro

 
Rais Kikwete akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa Umeme kutoka TANESCO

Rais Kikwete akiwa katika Hospitali teule ya Waso

Idd Uwesu, Arusha yetu
Jamii za wafugaji nchini zimetakiwa kubadili mfumo wa ufugaji wa mifugo na kuhakikisha zinanzisha ufugaji wenye tija na faida ili kujiletea maendeleo.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete alipokuwa anakamilisha uzinduzi wa zoezi la kutoa kifuta machozi kwa kaya zilizopoteza mifugo yao wakati wa ukame  katika miaka ya 2008/2009 wilayani Ngorongoro.
Rais Kikwete alisema kuwa jamii hizo hazina budi kubadilika na kuona umuhimu wa ufugaji bora kwa kuwa na mifugo ambayo mfugaji ataweza kuihudumia na kupata mazao bora ya mifugo hiyo.
Alisema kuwa katika kuhakikisha sekta hiyo ya ufugaji inakua nchini, Serikali imeandaa program maalumu kwa ajili ya kuendeleza mifugo na kwamba kazi hiyo imekwisha kinachosubiriwa ni uzinduzi rasmi ili kuhakikisha ufugaji bora kwa mazao zaidi.
Mara baada ya zoezi hilo Rais pia alipata nafasi ya kutembelea kituo cha Umeme cha Ngorongoro na Hospitali teule ya Wilaya ya Waso.
Akizungumzia kuhusu umeme Rais Kikwete amesema nia ya serikali ni kuona kila eneo nchini lina nishati ya umeme hivyo serikali inajitahidi kufanya kila linalowezekana ili maeneo mengi yapate nishati hiyo.
“Katika enao hili hivi sasa kuna umeme wa kutosha kazi iliyopo ni kuuasambaza  katika maeneo mingi zaidi” alisema Rais Kikwete
Nao baadhi ya wawakilishi wa kaya zilizopata ng’ombe hao wameishukuru Serikali kwa kuwasaidia mifugo hiyo na kusema kuwa itawasaidia kwa kuanzisha upya ufugaji baada ya kuwa katika wakati mgumu kwa kipindi chote tangu kutokea kwa ukame huo.
Ng’ombe zaidi  ya elfu 25 na mbuzi elfu 14 wanatarajiwa kugaiwa kwa kaya zaidi ya elfu 6 kutoka wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro mkoani hapa .
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa