Na Idd Uwessu, Arusha yetu Blog
WATANZANIA wameaswa kumrudia Mungu na kumuomba toba kwa ajili ya kuikomboa nchi kuondokana na magonjwa, umasikini na majanga mbalimbali.
Wito huo umetolewa na Muhubiri Jovin Msuya wa kanisa la Safina wakati akihubiria waumini wa kanisa hilo waliokusanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kufanya toba na kuliombea amani taifa ili kulikinga na majanga.
Msuya alisema kuwa kuwa matatizo yanayoikumba nchi yetu hivi sasa hayatakwisha endapo Watanzania hawatamamrudia mwenyezi Mungu na kuomba toba ya kweli.
Alisema pamoja na kufanya toba hiyo jamii haina budi kujitafakari juu ya mapito yake na kuachana na vitendo vyote vinavyo mchukiza muumba halia ambayo itaongeza neema na mafanikio ya kweli miongoni mwao.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment