Na Idd Uwesu (Arusha yetu Blog)
Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa PrecisionAir Bw. Alfonse Kioko alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha
Uduni wa miundo mbinu katika viwanja vya ndege na Gharama kubwa za uendeshaji wa usafiri huo vimetajwa kuwa sababu kubwa inayopeleka kuweko kwa gharama kubwa za nauli za ndege nchini.
Imeelezwa kuwa miundo mbinu mingi kwenye viwanja vya ndege ni mibovu na haikidhi mahitaji hali inayopelekea bei kuwa juu kutokana na gharama kubwa za uendeshaji.
Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa PrecisionAir Bw. Alfonse Kioko alisema hali hii kwa kiasi kikubwa inachangiwa na gharama kubwa za uendeshaji ambazo zinatokana na mfumo mzima wa uendeshwaji wa sekta hiyo huku akitole mfano wa viwanja vya ndege kufungwa nyakati za usiku na hivyo kuwalazimu kutofanya kazi nyakati hizo. Amesema nchi za ulaya na kwengineko wana viwango vidogo vya nauli kwa kuwa wanafanya kazi kwa masaa mengi hali inayowapatia mapato makubwa.

0 comments:
Post a Comment