Home » » TAKUKURU kujiunga IAACA kuwasaidia kujenga uwezo kukabiliana na Rushwa- Rais Kikwete

TAKUKURU kujiunga IAACA kuwasaidia kujenga uwezo kukabiliana na Rushwa- Rais Kikwete

Na  Mwandishi-MAELEZO-Arusha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete amesema  hatua ya Taasisi ya  Kuzuia
na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kujiunga na Mamlaka ya
kimataifa ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (IAACA) kutasaidia kupanua
wigo Taasisi katika kuimarisha mapambano dhidi ya rushwa nchini.
Rais Kikwete ametoa kauli hiyo leo(jana) jijini  Arusha wakati akifungua mkutano wa watendaji wakuu wa Taasisi za kupambana na Rushwa kutoa nchi mbalimbali Duniani.
Amesema
kuwa hatua hiyo ya TAKUKURU kujiunga na IAACA itawasidia kukabiliana na
vitendo rushwa kwa usaidizi wa kimataifa pindi watuhumiwa
wanapokimbilia Nchi nyingine kwa ajili ya kupata hifadhi ili
wasifikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Rais Kikwete amesema hatua hiyo itasaidia kuimarisha vita dhidi ya  baadhi
ya watendaji ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kujinufaisha na mali
za umma na hivyo kurudisha nyuma maendeleo katika baadhi ya miradi
ambayo ingetumia fedha fulani kuiendeleza badala inazoishia katika
mifuko ya watu wachache.
Hivyo  Rais Kikwete ametoa wito kwa  nchi wananchama kuisaidia TAKUKURU kwa fedha na vifaa kwa ajili ya kuwasaidia  katika vita dhidi ya kupambana na rushwa nchini.
Rais
Kikwete ameongea kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu katika kufanikisha
mapambano dhidi ya rushwa nchini ili vita hiyo iweze kuleta matunda na
tija kwa Taifa na wananchi wake .
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Dr. Edward Hoseah amesema kuwa mkutano huo
ambao unafanyika kwa mara ya kwanza nchini utasaidia kubadilishana
uzoefu na kuwajengea uwezo Nchi wananchama kwa ajili ya kuwa na mtandao
utakaosaidia utakaowaunganisha katika kukabiliana na vitendo vyote vya
rushwa katika maeneo yao.
Amesema kuwa hatua hiyo itasaidia misingi itakayowawezesha  kuwa na malengo ya pamoja na kampeni za pamoja  ya jinsi ya kukabiliana na rushwa ulimwenguni .
Aidha Dr. Hoseah amekiri  kuwa
pamoja jitihada kubwa zilizofikiwa na TAKUKURU katika kupambana na
rushwa bado rushwa ni changamoto kubwa ambayo inahitaji ushirikiana kwa
wadau wote ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi ili waweze kutoa ushirikiano
kwa Taasisi pindi wanapohitaji taarifa.
Amesema
kuwa kuiachia TAKUKURU pekee haiwezi kumaliza tatizo la uwepo wa rushwa
nchini na hivyo kuwataka wananchi wawe chachu ya kuimarisha mapambano
hayo.
Mkutano huo ni mara ya kwanza kufanyika nchini  ambpao zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi mbalimbali zinashiriki mkutano huo wa siku tatu.
Washiriki hao wanatoka  Nchi
za vile Morocco , Uingereza, Qatar, Uganda, Romania, Brazil, Austria,
india, Belgium , Spain, Ukraine , Malsiyia , Namibia na Mwenyeji
Tanzania.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri juu ya Rushwa ya Umoja wa Afrika kuanzia mwezi Machi mwaka huu.



0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa