Arusha
Home » » Shule zatakiwa kuanzisha somo la ujasiriamali

Shule zatakiwa kuanzisha somo la ujasiriamali

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
TAASISI za elimu nchini zimeshauriwa kuongeza mitaala ya ujasirimali shuleni ili kuwawezesha wanafunzi wanaomaliza masomo katika ngazi zote kuanzia shule za msingi na sekondari kuwa na uwezo wa kujiajiri bila kutegemea ajira za serikali.
Wito huo ulitolewa mjini hapa jana katika Shule ya Sekondari Ganako na mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Babson kilichopo Jimbo la Boston, Marekani, Profesa Dennis Hanno wakati akikabidhi vyeti vya uhitimu kwa  wanafunzi 119 kutoka shule tatu za sekondari mjini Karatu ambao walipata mafunzo ya ujasiriamali.
Mafunzo hayo yalitolewa na wanafunzi 10 wa Chuo Kikuu cha Babson kwa usimamizi wa mkufunzi huyo ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kama hayo ambayo wameyatoa Rwanda, Uganda na Ghana.
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa