Arusha
Home » » Mwanafaunzi atoa msaada kwa wanafunzi familia duni

Mwanafaunzi atoa msaada kwa wanafunzi familia duni

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Tangayika ya jijini Dar es Salaam, Ali  Jivraj,  ametoa msaada wa taa 200 zinazotumia nishati ya mwanga wa jua kwa wanafunzi waliotoka familia duni wa  kituo cha UAACC, kilichopo Embaseni, wilayani Arumeru, ili watumie kusomea ,uda wa saa za ziada.
Akizungumza  wakati akikabidhi taa hizo kwa wanafunzi wa kituo hicho, Jivraji alisema ameamua kutoa taa hizo kutokana na kuguswa na hali ya wanafunzi hao ambao wametoka familia zenye mazingira magumu na baadhi yao yatima.

Alisema kuwa kitu kilichomsukuma kutoa taa hizo ni baada ya kuona kutakuwa na tofauti kubwa ya watoto wa wenye uwezo kwa sababu ya kujisomea shule zenye nishati ya umeme wakati wote na hao kutosoma  usiku kwa kukosa nishati ya umeme.

"Taa hizi zinachajiwa kwa saa nne na zina uwezo wa kuwaka saa nne,  lakini pia zina uwezo wa kukaa miaka kumi bila kuharibika," alifafanua.

Alisema  ametoa taa hizo kwa ushirikiano na Hoteli ya Duble Tree ya jijini Dar es Salaam naye aliguswa kufanya hivyo. Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, alishukuru wahisani hao na kuomba wadau wa elimu kusaidia zaidi jamii  ya watu wasio na uwezo ili kuinua sekta ya elimu.

Mulongo alisema suala la elimu siyo la serikali peke yake na lina changamoto nyingi  hivyo wanahitaji kushirikiana na wadau kama hao kusaidia sekta hiyo.

"Sisi serikali tuna mambo mengi hatuna uwezo wa kufanya mambo mengi kwa mara moja, bali tunafanya kwa awamu na yeyote anayewaunga mkono anakuwa rafiki, lakini anayepinga maendeleo kwao ni adui,"alisema Mulongo.

Aidha,  alipongeza jitihada za kituo hicho kuwezesha watoto hao zaidi ya 22 kupata ujuzi wa ufundi  ili wanapomaliza masomo yao ya darasa la saba na sekondari wanakuwa na uwezo wa kujiajiri wenyewe kwenye ufundi wa aina mbalimbali.

Kwa upande wake, Meneja wa kituo hicho cha UAACC, Christopher Nnko, alisema kuwa msaada huo ni mkubwa kwao kwani utapandisha ufaulu kwa watoto wao.

Alisema kituo hicho kilianza mwaka 1991 na lengo la kuanzishwa kwake lilikuwa kusaidia watoto wanaotoka jamii isiyo na uwezo na tayari wana jumla ya watoto 22 waliotoka katika jamii hiyo inayozunguka eneo hilo.

"Lakini watoto hawa wapo wanaolala hapa ambao familia zao hazina uwezo kabisa na hivyo wao wanawapatia elimu na mafunzo ya kompyuta, uchoraji na vitu vingi vya ufundi ili wanapomaliza wajiajiri wenyewe," alisema Nnko.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa