Na Pamela mollel, Arusha
Katika kukuza utalii hapa nchini,Zanzibar na Mkoa wa Arusha yaungana kukuza soko la utalii kimataifa na kutanua wigo kwenye eneo la Utalii wa Urithi,Utalii wa michezo na Utalii wa afya kupitia msimu wa kwanza wa Tamasha la Utalii na Uwekezaji Zanzibar utakaofanyika Oktoba 25-26 mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari,katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Aris Abbas Manji,anasema ujio wao Arusha ni kutangaza Tamasha hilo la utalii na uwekezaji kwa wadau wote wa utalii ili waweze kushiriki katika Tamasha hilo
Ameongeza kuwa Uchumi wa Zanzibar umekuwa ukichangiwa na sekta ya utalii kwa asilimia thelasini ambapo wameweza kutanua wigo wa bidhaa za utalii
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Poul Makonda amepongeza ujio huo wa Tamasha la kwanza la utalii na uwekezaji Zanzibar,ambapo ameeleza kuwa Mkoa wa Arusha upo bega kwa bega na Zanzibar katika kuhakikisha wanachochea na kutengeneza mazingira mazuri katika sekta ya utalii ili kuwavutia Wageni wengi zaidi na kutoa ajira kwa vijana.
0 comments:
Post a Comment