Home » » DKT.ABBAS APONGEZA UTAFITI ULIOFANYWA NA MISA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA CPESA

DKT.ABBAS APONGEZA UTAFITI ULIOFANYWA NA MISA TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA CPESA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas,akizungumza na Maafisa Habari, Asasi za Kiraia pamoja na  waandishi wa habari  wakati kupokea taarifa ya   mrejesho wa utafiti uloiofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na CIPESA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa MISA Tanzania Bw.  Gasirigwa Sengiyumva akiuliza maswali wakati wa mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.


Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania Bw. James Marenga akitoa mrejesho wa utafiti uloiofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na CIPESA kwa Maafisa Habari wa Serikali, Asasi za Kiraia pamoja na Waandishi wa Habari Jijini Arusha.
Bi. Ashnah Kalemera kutoka CIPESA akiwasilisha mambo mbalimbali yanayohusiana na upatikanaji wa Taarifa katika ukanda wa Afrika Mashariki


Bi. Juliet Nanfuka kutoka CIPESA akizungumza jambo wakati wa kupokea taarifa ya utafiti iliyofanywa na MISA Tanzania kwa kushirikiana na CIPESA


Baadhi ya wadau mbàlimbali pamoja na waandishi  katika mkutano huo


Mwandishi wa Gazeti la Habari leo Veronica Mheta akichangia mada katika mkutano huo


Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO)  Bw. Paschal Shelutete akijibu maswali mbalimbali wakati wa  mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda


Kaimu mkurugenzi wa MISATAN nchini Gasirigwa Sengiyumva (wa kwanza kushoto)akiwa na mmiliki wa Wazalendo Blog,Gadiola Emmanuel (mwenye skafu nyekundu shingoni) wakati wa kusikiliza wadau wanatarajia nini baada ya kusikiliza ripoti ya utafiti.
Mwenyekiti wa MISA Tanzania Bi. Salome Kitomari akitoa neno la Shukurani ikiwa ni pamoja na kumshukuru Msemaji Mkuu wa Serikali Hassan Abbas kwa ushiriki wake,Maafisa habari mbalimbali wa Serikali, Wadau kutoka Asasi za Kiraia pamoja na waandishi wa Habari.



 Mafunzo yakiendelea katika Hotel ya Impala Jijini Arusha.




Na.Vero Ignatus Arusha.



MSEMAJI Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas amesema Maafisa Mawasiliano serikalini bado wanakabiliwa na changamoto kutoka kwa mabosi wao, ikiwano wengine kutokutaka habari zao zisikike kwenye vyombo vya habari.



Dkt.Abbas aliyasema hayo jana mjini hapa wakati mapitio ya ripoti ya upatikanaji wa Taarifa Tanzania uliofanywa na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika(MISATAN) ikishirikiana na Taasisi ya CIPESA ya nchini Uganda.



Alisema kupitia ripoti hiyo aliyoiunga mkono na kuisoma vyema atahakikisha maofisa mawasiliano zaidi ya 300 wanaokutana mjini Arusha wanapata utafiti huo."Nimesoma utafiti huu, kurasa zote upo vizuri, niwaombe muendelee kufanya tafiti kama hizi kwani ni chakula kwetu," alisema Dkt. Abbas.



Akizungumzia utafiti uliofanywa katika mikoa 7 na MISATAN Wakili wa mahakama kuu James Marenga amesema ofisi za halmashauri ya mikoa ya Arusha na kigoma ,walau ndiyo zimeonekana ndiyo wanafanaya vizuri katika kuwa wazi katika utoaji wa taarifa kuliko ofisi za mikoa.



Dodoma manispaa,halmashauri ya Jiji la mbeya,Kigoma ofisi ya mkuu Arusha, ofisi ya mkuu wa mkoa Mwanza hakukuwa na ushirikiano,vilevile mkoa wa Mtwara hakukuwa na ushirikiano ,Dar ni katika halmashari ya Jiji,Kwahiyo Utafiti huo ulikuwa umegawanya utoaji  wa taarifa kwa ofisi za mkuu wa mikoa na ofisi za halmashauri au za Majiji katika mikoa iliyochaguliwa.



Moja ya mapendekezo yaliyotolewa baada ya utafiti huo vitengo vya watoa taarifa vinaimarishwa kama inavyotakiwa  katika sheria ya haki  kupata taarifa ya mwaka 2016.Vilevile utafiti huo unasisitiza kuwepo na uwazi katika utoaji wa taarifa haswa kwenye taasisi za serikali.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa