Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda mara baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere
wakati akielekea kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara
ya kikazi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam katika
Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akielekea
kupanda ndege kwenda mkoani Arusha kwa ajili ya ziara ya Kikazi. PICHA
NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo
tarehe 20 Septemba, 2017 ameondoka jijini Dar Es salaam kuelekea mkoani
Arusha kwa ziara ya kikazi.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA,Rais Dkt. Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Manyara kwa kufungua barabara ya Kia - Mererani yenye urefu wa kilomita 26, na kuzungumza na wananchi wa mkoa huo.
Tarehe 23 Septemba 2017, Rais Dkt. Magufuli atatunuku Kamisheni kwa Maafisa wanafunzi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.
Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar Es salaam , Rais Dkt. Magufuli ameagwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe. Paul Makonda.
Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es Slaam.
20 Septemba 2017.

0 comments:
Post a Comment