Home » » WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

WAZIRI MHAGAMA AZITAKA HIFADHI ZA TAIFA KUTUMIA WASANII KATIKA KUTANGAZA VIVUTIO VYA UTALII

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama akiwa anamsikiliza Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto mara baada ya kuwasili katika banda hilo hivi karibuni jijini Arusha katika maadhimisho ya sikukuu ya nane nane


Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania.
Na Pamela Mollel,Arusha

WAZIRI wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Jenista Mhagama amezitaka hifadhi za taifa nchini kuendelea kuwatumia wasanii nchini katika kutangaza vivutio mbalimbali vinavyopatikana huku akiipongeza Mamlaka ya hifadhi za taifa Ngorongoro inavyotangaza vivutio vyake kupitia msanii Mrisho Mpoto.


Kauli hiyo aliitoa hivi karibuni  jijini Arusha alipotembelea banda la Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro katika maonesho ya Nanenane.

Alisema kuwa wasanii wananafasi kubwa ya kuutangaza utalii wa ndani na kuendelea kuitangaza Tanzania endapo watatumiwa kama mabalozi kupitia umaarufu wao jambo ambalo litasaidia pia kuiingizia nchi kipato kupitia watalii.

Naye Balozi wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Mrisho Mpoto aliwapongeza watanzania kuwa na mwitikio mkubwa wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kuwapeleka watoto wao katika maonesho hayo ili kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na mamlaka hiyo hivyo kuwaandaa watoto hao kuwa wahifadhi kwa baadae.

"Mfano mzuri ni hili la punguzo la shilingi elfu 50 lililotolewa ili watanzania waweze kutembelea hifadhi ya Ngorongoro tumeona watu walivyochangamkia na kwenda kutembelea Ngorongoro  hivyo ni jambo zuri na la kupongezwa kwa watanzania  na ninaomba waendelee kutembelea hifadhi zetu"alisema Mpoto.

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro Peter Makutian aliwashukuru watanzania kuendelea kuhamasika kutembelea hifadhi hiyo tofauti na awali na kusema kuwa idadi ya wageni toka nje ya nchi wanaotembelea hifadhi hiyo kwasasa ipo sawa na watanzania.

Aidha aliwaomba watanzania wengine kuendelea kutembelea vivutio vya Tanzania ikiwemo Ngorongoro kwakuwa gharama wanazotoza ni ndogo kwao ukilinganisha na wageni toka nje ya nchi hivyo ni fursa nzuri kwao kuitumia na kuwa mabalozi wa hifadhi kwa wengine.





0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa