Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesababu za serikali na maoni yake iliyoangalia maeneo matatu ya ripoti hiyo
Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya Taasisi ya wajibu.
Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert akizindua ripoti ya taasisi ya wajibu leo jijini Dar es Salaam.
Picha pamoja Mkuu wa Program ya uwajibikaji wa masuala ya fedha Tanzania wa Shirika la Maendeleo ya Ujerumani, Dk. Annette Mumert, Watendaji wa Taasisi ya wajibu pamoja na wadau mbalimbali.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .
Taasisi
ya Wajibu imezindua Ripoti ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016 katika maeneo ambayo
ni muhimu kwa kila mtanzania kuweza kujua ripoti hiyo kwa mstakabali wa
maendeleo ya taifa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kabla ya uzinduzi
huo Mkurugenzi Mtendaji Taasisi hiyo, Lodovick Utouh amesema kuwa ripoti
hiyo imeangalia maeneo matatu ya Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa Hesabu za
Serikali (CAG) na maoni yake katika ukaguzi wa 2016 ambayo ni Serikali
Kuu, serikali za Mitaa pamoja na Mashirika ya Umma.
Amesema
kuwa katika ripoti hiyo kwa deni la taifa linatakiwa kwa serikali
kuongeza vyanzo vya mapato ili kuweza kulipa na shughuli zingine za
maendeleo ziendelee bila kuongeza mapato na kulipa deni kutafanya
shughuli hizo za maendeleo kukwama.
Utouh
amesema katika ripoti hiyo agizo la serikali kwa Halmashauri kutenga
asilimia 10 ya kuwawezesha vijana na wanawake inatakiwa kuwa ni mikopo
wanayopata inatakwa kuwa katika mzunguko na kuweza kila mtu kumfikia
mkopo huo.
0 comments:
Post a Comment