Home » » MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO ASHIRIKI UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI KATIKA KITUO CHA AFYA CGA MTO WA MBU

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO ASHIRIKI UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI KATIKA KITUO CHA AFYA CGA MTO WA MBU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akishiriki ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo cha afya cha Mto wa Mbu.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha akibeba tofauli kama ishara yakuwaunga mkono wananchi wa mto wa mbu katika ujenzi wa jengo la upasuaji.Wanakijiji wa tarafa ya Makuyuni wilayani Monduli wameungana na halmashauri yao katika kujenga jingo la upasuaji, na maabala yakisasa katika kituo chao cha afya cha mto wa mbu.

Akitoa pongeza kwa jitihada hizo Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo amewapongeza kwa jitihada hizo kwani imekuwa ni mfano wakuigwa kwa wananchi wote wa Mkoa wa Arusha kushirikiana na serikali yao katika shughuli mbalimbali zakuleta maendeleo.

“Nimefararijika sana kujiunga nayi katika ujenzi huu wa chumba cha upasuaji na maabala yakisasa, hivi ndivyo viongozi tunapaswa kushirikiana na wananchi katika kufanya shughuli za maendeleo badala yakuwa wasimamizi inabidi tuonyeshe mfano”.

Gambo aliendelea kutoa msisitizo zaidi kwa viongozi wengine kuacha tabia yakuwa wasimamizi huku wakitoa maelekezo badala yake waonyeshe mfano kwa kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo ya wananchi wao.

Aidha mbali nakushuriki ujenzi huo Gambo alitoa ahadi yakuchangia mabati mia na mifuko ya simenti mia ili isaidie katika kuendeleza ujenzi wa jengo hilo.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta alisema juhudi za ujenzi huo niwa vijiji vya Kigongoni,Baraa na Esilalei ambao wanachangia ujenzi huo huku halmashauri ikiwa imechangia milioni nane na jumla ya gharama ni milioni 145.

Hata hivyo amesema ofisi yake itachangia  milioni 2 za ujenzi wa jengo hilo na kuaidi kufikia mwezi wa sita mwaka huu jengo hilo litakuwa limeisha au linakaribia kuisha ili wananchi waweze kuanza kulitumia.

Akisisitiza zaidi mbunge wa jimbo la Monduli Julias Laiza amesema nivizuri viongozi na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za maendeleo ya wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao na wao kama viongozi wameshiriki pia katika ujenzi huo,naye akaadi kuchangia milioni 1 kama kianzio ila ataendelea kuchangia mpaka ifikia kiasi cha milioni 5.

Akimalizia kwa kutoa pongeza za juhudi hizo mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli Isack Joseph amewata wananchi wote wamuunge mkono mkuu wa mkoa Gambo kwa juhudi za maendeleo anazozionyesha kwa mkoa huu na halmashauri yake itachangia milioni 10 kwenye ujenzi huo.

Wananchi wa mto wa mbu wamekuwa wakipata shida zakupata huduma za afya hususani huduma ya upasuaji hasa kwa wanawake wajawazito nakuwalazimu kusafiri umbali mrefu kwenda Monduli mjini au Karatu lakini kwa ujenzi huo utakuwa msaada mkubwa sana kwao.


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa