Home » » MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA

 
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, amefanya mazungumzo na ujumbe kutoka  nchini China , waliotaka kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo Mkoani Arusha,mzungumzo hayo yalifanyika ofisini kwake..
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akipeana mkono na Mjumbe kutoka ubalozi wa China nchini,Gou Huodong kama ishara yakuonyesha ushirikiano baina ya nchi ya China na Mkoa wa Arusha.
 
Amewahakikishia kuwapa ushirikiano,mazingiza mazuri  na usalama kwa wawekezaji kutoka China watakaofika kuwekeza katika Mkoa wa Arusha, na watakapoitaji msaada wowote kutoka Serikalini basi watapatiwa kwa wakati.
“Kwa Mkoa wa Arusha mtapata ushirikiano wakutosha kutoka Serikali na mtakapoitaji msaada sehemu yoyote katika utendaji wenu wa kazi basi msisite kuwasiliana nasi na tutawasaidi”,alisema Gambo.
Aidha mjumbe kutoka ubalozi wa China kwa Tanzani bwana Gou Huodong,amemwakikishia Muheshimiwa Mkuu wa Mkoa kuwa ataenda kuwahamasisha wachina wengine waliopo China kuja kuwekeza zaidi Mkoani Arusha hasa kwenye sekta ya Utalii ambayo ndio inayokuwa kwa kasi sana na inaongeza pato la taifa kwa asilimia kubwa.
“Nitaenda  kuwahamasisha wenzangu huko China waje kwa wengi hapa Mkoani Arusha kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbalia hasa ya Utalii kwasababu sekta hii inakuwa kwa kasi sasa,”alisema Gou.
Pia Muheshimiwa Gambo aliwaelezea mpango wakufunga Kamera za barabarani(CCTV) kwa Mkoa wa Arusha ilikuimalisha zaidi ulinzi na Usalama hasa kwa wawekezaji na watalii wanaoingia katika Mkoa huu, na hivyo kuwaomba waangalie hiyo fursa kwa upande wao iliwaisaidie Serikali katika kuimalisha ulinzi wake maeneo mbalimbali ya Mkoa.
Ugeni huu kutoka ubalozi wa China hapa nchini ulikuwa na lengo kubwa lakuweza kufahamu maeneo mbalimbali ya uwekezaji yaliyopo katika Mkoa wa Arusha, kwakuwa wageni wengi kutoka China waliofika katika Mkoa wa Arusha walikutana na mazingira mazuri ya uwekezaji.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa