BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) mkoani hapa, limeitaka
jamii nchini kuhakikisha inaangalia familia zilizoachwa na wazazi wao na
kuishi kwenye mazingira magumu zisaidiwe ziweze kujikimu kimaisha.
Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Shehe
Mohamed Maviwa wakati akikabidhi msaada wa vifaa vya ushonaji kwa
msichana Amina Mohamed (20) wa Sombetini anayetokea katika familia
inayoishi kwenye mazingira magumu.
Alisema ni jukumu la jamii kuhakikisha inazisaidia jamii zenye
mahitaji maalumu kwani zimekuwa zikikabiliwa na changamoto mbalimbali na
mwisho wa siku watoto kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa.
“Kuna jamii nyingi ambazo zinakabiliana na changamoto mbalimbali
kutokana na familia nyingi kuathirika kwa kuachwa na kubakia masikini
hatua ambayo inachangia watoto kuishia kukaa mtaani kujiingiza kwenye
makundi yasiyofaa,” alisema Maviwa.
Naye Katibu wa Bakwata Mkoa wa Arusha, Abdalah Masood alisema
wamefikia hatua ya kumsaidia mtoto huyo kutokana na changamoto
zinazomkabili ikiwamo kuwa na jukumu la kulea wadogo zake na mama yake.
“Naiomba jamii isaidie jamii zenye mahitaji kama hizi kwani zimekuwa
na changamoto nyingi kutokana na kukosa msaada,” alisema Masood.
Kwa upande wake, Amina aliwashukuru kwa msaada huo kutokana na
changamoto mbalimbali zilizokuwa zikimkabili ikiwamo ukosefu wa vifaa
vya ushonaji pamoja na kuwa na ujuzi huo.
Alisema, bado anakabiliwa na changamoto ya sehemu ya kushonea hivyo
aliomba wadau mbalimbali kumsaidia ili aweze kupata eneo na hatimaye
kuendeleza biashara yake.
Chanzo Gazeti la Habari leo
0 comments:
Post a Comment