Arusha
Home » » KINANA AKUMBUSHWA AHADI KWA WAFANYAKAZI WA KILTEX.

KINANA AKUMBUSHWA AHADI KWA WAFANYAKAZI WA KILTEX.

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WALIOKUWA wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Kiltex cha jijini hapa, ambao waliachishwa kazi miaka zaidi ya 20 iliyopita, wamemkumbusha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana kuwasaidia kupata haki zao.
Wafanyakazi hao waliyaeleza hayo juzi jijini hapa walipokuwa wakizungumza na vyombo vya habari kuelezea kutokulipwa mafao yao tangu kuachishwa kazi zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Mwenyekiti wa wafanyakazi hao, Rajabu Madambo, na Katibu wake, Nathaniel Longido, walisema kwa nyakati tofauti kuwa Desemba, 2014, walimpatia Katibu Mkuu Kinana barua ya kuomba awasaidie kufikisha kilio chao serikalini ili walipwe stahiki, lakini hadi leo hawajalipwa.
Madambo alisema, wamelazimika kumkumbusha Kinana kwa kuwa alionesha dalili za kuwasaidia kufikisha suala lao kwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete wakati huo na sasa wanamuomba afikishe kwa seikali iliyopo madarakani walipwe.
Alisema waliachishwa kazi baada ya kiwanda hicho kusitisha shughuli zake na barua za kuwaachisha zilieleza wangelipwa stahiki zao ikiwemo kiinua mgongo, kurejeshwa makwao, kukatishwa mkataba, mambo ambayo hayajafanyika.
Mwenyekiti huyo alisema Desemba 2014, Kinana alifanya ziara wilayani Arusha na alipita kwenye kiwanda cha Kiltex, ambapo walimkabidhi barua ya kuomba serikali iwalipe mafao yao.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati hiyo, Juma Mgosi alisema, baadhi ya wafanyakazi wameshafariki bila kulipwa stahiki zao.
Alisema, kuachishwa kazi kuliwaathiri kimaisha, na kiuchumi kwa kuwa walishindwa kuwa na malengo mazuri ya kuziendesha familia zao, hivyo kupoteza mwelekeo wa maisha. Aliongeza kuwa, kutokana na ucheleweshaji huo wa malipo, wanamuomba Rais Magufuli asikilize kilio chao.
 CHANZO : HABARI LEO.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa