Home » » Madiwani Arusha watimkia Chadema

Madiwani Arusha watimkia Chadema

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

  Ni kutokana na kuchoshwa na mwenendo wa kura za maoni kutawaliwa na rushwa ndani ya chama
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeendelea kupata pigo baada ya waliokuwa madiwani wake wanne wa Halmashauri ya Meru, Mkoa wa Arusha kukihama na kujiunga na Chadema.
Waliohama ni  Loth Nko wa Kata ya Maji ya Chai, Godfrey Kishongo wa Kata ya Nkoaranga, Abraham Kaaya kutoka Kata ya Maroroni na Mwanaidi Kimu wa Kata ya Makiba.

Wakitangaza uamuzi wa kukihakama CCM mbele ya mgombea ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) jana, madiwani hao walielezea kuchoshwa na CCM, hususan, kuhusu mwenendo wa kura za maoni ndani ya chama hicho waliodai kutawaliwa na vitendo vya rushwa.

Walisema hawapo tayari kufanya kazi ndani ya CCM baada ya chama hicho kumkata Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, katika kinyang’anyiro cha urais. Jumatano iliyopita, Nassari aliwapokea na kuwapa kadi aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro, Elias  Ngorisa kwa niaba ya madiwani wenzake 18.

Diwani wa Kata ya Engusero Sambu, Kagil Mashati Ngukwo, ambaye pia alikuwa Katibu wa Fedha na Uchumi wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, alikuwapo pamoja na wazee wa mila wa kabila la Wamasai (malaigwanani), Laurence Ngorisa na Lekakui Oleiti, wote kutoka Engusero Sambu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa