Home » » BALOZI MDOGO WA KENYA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA SIMBA CEMENT KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA‏

BALOZI MDOGO WA KENYA NCHINI TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA SIMBA CEMENT KATIKA MAONYESHO YA NANE NANE ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

IMG_1853Aliyevalia shati la blue ni Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia akiondoka katika banda la kampuni ya Simba Cement mara baada ya kutembelea banda hilo katika viwanja vya nane nane Themi jijini Arusha ,kushoto ni Mkurugenzi wa Kenya plant helth inspectorate service Bi.Esther Kimani(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
IMG_1863Wananchi wakipata elimu katika banda la Simba Cement katika maonyesho ya nane nane ya kandaele ya kaskazini yanayoendelea katika viwanja vya njiro Themi jijini Arusha
IMG_1851(1)Ugeni kutoka kenya wakiongozwa na Balozi mdogo wa Kenya Tanzania,Boniface Muhia wakipata maelezo katika banda la Simba Cement
SAM_4855Afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement Leslie Massawe kushoto akitoa maelezo kwa mteja aliyefika katika banda lao katika maonyesho ya nane nane
SAM_4853
Tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya watumiaji wa saruji hapa nchini hawafati viwango vilivyowekwa na hivyo hupelekea kupata bidhaa isiyo bora kwa watumiaji wa bidhaa hiyo

Hayo yamebainishwa na afisa masoko Mkuu wa kampuni  ya Simba Cement ambao ni watengenezaji wa Saruji  ,Leslie Massawe wakati akitoa elimu kwa wananchi waliotembea banda lao katika maonyesho ya nane nane ,kanda ya kaskazini  jijini Arusha

Massawe alisema kuwa utafiti uliofanywa na kampuni yao ya saruji inaonyesha kuwa baadhi ya wajenzi hawafuati  mchanganyiko unaokubalika baina ya saruji,mchanga,kokoto hivyo inapelekea kupata matofali yaliyochini ya kiwango

“Bidhaa zetu ni matokeo ya utafiti wa kina na uboreshaji makini unaofanywa na wataalumu wetu kupitia ujuzi wao wenye sifa zinazozingatia viwango vya ubora wa simenti Tanzania”alisema Massawe

Aidha alisema kuwa wanautarabu wa kutoa elimu ya mara kwa mara kwa wateja wao pamoja na wananchi kwa ujumla juu ya matumizi sahihi ya saruji ,katika ujenzi wa sekta mbalimbali sanjari na uzalishaji wa viwandani hali itakayosaidia upatikaniji wa ujenzi wa nyumba imara na miundombinu bora

Alitoa wito kwa wananchi kupata elimu ya matumizi bora ya vifaa vinavyotumika katika ujenzi kabla ya kuanza ujenzi,huku akiwataka mafundi ujenzi  na watengenezaji wa matofali kutenga muda wa kushiriki semina mbalimbali zinazotolewa na kampuni za saruji

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa