Home » » TUKIO LA UZINDUZI WA SAMSUNG 'MUVIKA' 4G LTE ARUSHA‏

TUKIO LA UZINDUZI WA SAMSUNG 'MUVIKA' 4G LTE ARUSHA‏


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

UZINDUZI WA ‘SAMSUNG MUVIKA 4G LTE’ ARUSHA

Arusha, 29 Mei 2015. Nguli wa vifaa vya umeme Samsung imeendelea na juhudi za kuimarika katika nafasi ya kwanza kwa uzinduzi wa simu zake mpya na za kushangaza za 4G LTE zilizopewa jina la ‘Muvika’. Uzinduzi huu wa mara ya kwanza na wa aina yake nchini kwa upande wa simu za mkononi zenye teknolojia ya aina hii ulifanyika Hoteli ya Bay Leaf Arusha. Pamoja na utambulisho huo tukio lilikuwa kama jukwaa la usimamizi wa wazalishaji simu kukutana na wafanyabiashara wa hapa nyumbani, mawakala na wadau wengine muhimu.
Soko la simu za mkononi Arusha ni moja kati ya yale ambayo kampuni inayatazama kama fursa ya pekee na ilikuwa sababu ya kuchagua Arusha kwa uzinduzi wa 4G LTE mbali na Dar es Salaam. Kutokana ukuaji wa uchumi mkoani hapa na sekta kama za utalii na madini zinazosaidia katika maendeleo ya kiuchumi makampuni mengi kama Samsung yanakuja kwa kasi kuhakikisha huduma/bidhaa zao haziko mbali na wateja wao muhimu.
Uzinduzi ulifanyika mbele ya wageni waalikwa kutoka mkoani hapo kukiwa na burudani ya moja kwa moja kutoka kwa ‘msanii maarufu’ na balozi wa kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung Tanzania Vanessa Mdee.
Akiongea wakati wa sherehe za uzinduzi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya vifaa vya umeme ya Samsung Tanzania Bw Hyeongjun Seo, aliongelea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya kampuni na watu wa Arusha na umuhimu wa kuzingatia huduma bora na bidhaa inayoendana na Samsung. Alisema “Arusha ni mkoa muhimu kibiashara na hatuangalii tu kuendelea kutoa ubora wa uzoefu wetu kwa wateja lakini pia kuwapa bidhaa za kisasa na za kibunifu zinazoendana na soko la kimataifa.” 
Maoni ya Mkurugenzi mtendaji yaliungwa mkono na Sylvester Manyara, Mkuu wa Mauzo na Usambazaji Samsung Electronics Tanzania akisema “Leo tunazindua teknolojia hii katika uwepo wa mawakala na wasambazaji wetu, tumechagua Arusha ikiwakilisha nia ya kuendelea kukua ambako ni sehemu ya utamaduni wa Samsung.” 
‘Muvika’ ni neno lisilo rasmi linalojaribu kuelezea uwezo wa simu hii na wepesi wake katika mtandao unaokuja na 4G LTE unaowawezesha watumiaji kupata hadi filamu kwa kasi ya kushangaza. 4G LTE (Mabadiliko ya Kudumu ya Kizazi cha Nne) ni simu yenye teknolojia ya kisasa katika mtandao inayoipeleka Dunia kwa kasi. Kwa mahitaji yanayoongezeka ya simu za kisasa zenye uwezo kama huu Samsung Tanzania wanahakikisha kuwa mahitaji ya wateja wao yanafikiwa.
Akiwa kama balozi wa bidhaa za Samsung Tanzania Bi Vanessa Mdee atakuwa kama uso wa simu zitakazotolewa chini ya mwamvuli wa Muvika. Akichangia juu ya wajibu wake Vanessa alisema “Huu ni ukurasa mwingine mzuri zaidi tunaoufungua na Samsung tangu tulipoianza safari yetu pamoja na kama mzaliwa wa Arusha nafurahi kupata fursa hii kuwa mstari wa mbele wa mabadiliko ya teknolojia ambayo Samsung wanaanzisha”
Mwisho
Kuhusu Vifaa vya kielektroniki vya Samsung
Teknolojia ya Samsung inatumiwa na watu takribani 236,000 katika nchi 79, inaleta mabadiliko na kuiwezesha dunia kuingia kwenye teknolojia mpya na matumizi ya smart phone, luninga, air-conditioner, vifaa vya nyumbani vya kieletroniki, kamera, na vifaa vya maofisini kama kompyuta na printers ambavyo vina teknolojia ya hali ya juu kukidhi mahitaji ya wateja. Kujifunza mengi zaidi, tembelea www.samsung.com na www.facebook.com/SamsungMobileTanzania


HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI
Mabibi na Mabwana,
Waheshimiwa wageni waalikwa,
Wanahabari,
Na wafanyakazi wa Samsung
Habari za jioni,
Nawashukuru kwa kukubali mualiko wetu na kujiunga nasi katika hafla hii nzito. Ni fahari kuuona umati huu kwa mara nyingine tena.

Ningependa kuanza kwa kuwashukuru washiriki wetu waaminifu kwa michango yenu kwa mwaka mzima katika kuifanya Samsung kua na mwelekeo wa mafanikio mkoani hapa.

Kama ambavyo wote mnaweza kushuhudia, soko la simu za kisasa linakuwa duniani kote na hasa zaidi barani Africa
Tanzanian kama ilivyo nchi za jirani imeonesha sifa za kufanana. Pamoja na kuwa na wakazi wenye kipato cha kati mahitaji ya vitu vya kisasa kama simu za mkononi umekuwa mkubwa.

Na kwanini tusiwe sehemu ya mitindo ya kimataifa.
Ukuaji wa Uchumi wa taifa unaweza kuonekana kwa kiasi kikubwa katika shughuli mbalimbali zinazofanyika katika mkoa wa Arusha. Pamoja na utalii kuwa mchangiaji mkubwa wa uchumi wa nchi watu na wafanyakazi wa Arusha kama walivyo wengine wanastahili kufurahi.

Mabibi na Mabwana,
Leo tunakusanyika tena tunapoitambulisha bidhaa nyingine ya Samsung ambayo ina nia ya kubadili muelekeo wa shughuli za kila siku za wateja wetu.

Nani zaidi wa kusherehekea pamoja nao uzinduzi huu zaidi ya ninyi mawakala ambao mmekuwa wa muhimu katika kuhakikisha bidhaa zetu zinawafikia wateja wa Arusha pamoja na kudumisha ubora wa bidhaa na huduma zetu. Uwepo wetu uliodumu katika mkoa huu unaletwa na dhamira yetu ya dhati kumuwezesha kila mmoja kumiliki bidhaa yetu na jitihada za kuendelea kutoa ufumbuzi wa kibunifu unaoendana na soko la kimataifa.

Kwa simu zetu za MUVIKA tunatoa nguvu ya kasi zaidi kwa mteja wetu. 4G LTE inawakilisha hatua nyingine kwenye maendeleo ya simu za mkononi ikija na uwezo wa kasi zaidi katika mtandao yote ndani ya simu yetu hii. Huu ni uzinduzi wa kwanza wa aina yake Tanzania na tunaona fahari kuwa wa kipekee zaidi katika kuhakikisha kila mmoja anakuwa vizuri zaidi katika kupambana na changamoto za ulimwengu wa kisasa. 

Mabibi na Mabwana,
Kwa maneno hayo machache, naacha jukwaa wazi kwa ajili ya wenzangu kuwaelezea mengi zaidi juu ya Muvika na Samsung 4G LTE

Asanteni wote kwa mara nyingine kwa kukubali mualiko wetu na kutuazima muda wenu wa thamani zaidi kwenye tukio hili linaloendelea. Natazamia kukutana na kila mmoja wenu katika usiku huu.
Asanteni.


 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa