Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
TAMASHA
la Jambo Fashion Affair linatarajia kufanyika leo Jijini hapa na
kushirikisha wabunifu wa ndani pamoja na wasanii kutoka Jijini Arusha na
mikoa mbalimbali.
Akizungumzia maandalizi ya
tamasha hilo linafanyika leo, Augustine Namfua ambaye ni Mwenyekiti wa
Jambo Festval alisema wamaejiandaa vizuri kuhakikisha wananchi
wataohudhuria wanapata burudani ya ubunifu wa mavazi sambamba na muziki.
Alisema wabunifu mbalimbali
watakuwepo kama An Nisa, Fatma Naeem, Martin Kadinda ,Wanyoke Lewis,
iheartz Collection, Ankara By Chimzy, Fabilouskitenge, Zakia Collection,
gLushaju Clothing, Florinyah Designs ,Martin Mukiwa na wengine ambao
wataonyesha aina mbalimbali za mavazi.
Namfua alitumia nafasi hiyo
kuwasihi watanzania hususan wakazi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa
wingi katika tamasha hilo ambalo linafanyika leo Viwanja vya Allliance
Franc’aise Arusha na kiingilio kikiwa ni h, 20,000 kwa kila mtu.
“Tamasha hili tunalifanya kwa mara
ya nne na wasanii mbalimbali pamoja na wabunifu wa mavazi wataonyesha
ubunifu wao katika tamasha hili hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa
wingi kwani mbali na maonyesho ya mavazi pia kutakuwa na burudani za
aina mbalimbali sambamba na vinywaji”.
Naye Meneja Mauzo wa kampuni ya
Megatrade Investment Ltd, Edmund Rutaraka alisema kampuni hiyo ndio
wadhamini wa tamasha hilo na pia watatoa huduma mbalimbali za vinywaji
ili kufanikisha tamasha la ubiifu huku Mkurugenzi wa Alliance Francaise
kutoka Arusha, Ga’’ele Lapostolle akisema taasisi yao imeamua
kushirikiana na wahusika wa tamasha hilo ili kukuza utamaduni wa
watanzania sambamba na ubunifu wa mavazi pamoja na muziki ambao ni ajira
kwa vijana.
Naye mmoja kati ya wanamuziki
kutoka Jijini arusha ambaye atashiriki katika tamasha hilo na kukonga
nyoyo za washiriki wa tamasha hilo, Elisha Simon maarufu kama Hisia
aliwasihi wakazi wa Ausha kujitokeza kwa wingi kuona vipaji vya wasanii
pamoja na mavazi yatakayoonyeshwa katika tamasha hilo.

0 comments:
Post a Comment