Arusha
Home » » SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 14.5 WA KULINDA MAZINGIRA,KUKUZA UHIFADHI NA UTALII NCHINI TANZANIA‏

SERIKALI YA MAREKANI YAZINDUA MRADI WA DOLA MILIONI 14.5 WA KULINDA MAZINGIRA,KUKUZA UHIFADHI NA UTALII NCHINI TANZANIA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
SAM_3286 
Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa PROTECT  wa dola za kimarekani Milioni 14.5 wa kulinda mazingira,kukuza uhifadhi na utalii nchini hapa unaolenga kujenga uwezo wa uhifadhi na kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori nchini kote Tanzania,uzinduzi huu ulifanyika jana katika eneo la hifadhi ya wanyamapori linalosimamiwa na jumuiya ya uhifadhi ya wanyamapori {WMA} la Randilen linalopakana na hifadhi ya taifa tarangire Wilayani Monduli mkoani Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_3306
Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress wakitiliana saini mkataba wa mradi wa PROTECT na Waziri wa Mali Asili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu
SAM_3297
Waziri wa Mali Asili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu akizungumza katka uzinduzi huo, ameishukuru serikali ya Marekani kwa msaada huo huku akiongeza kuwa kumekuwa na uvamizi mkubwa katika maeneo ya hifadhi za taifa na kusema kuna mpango makakati wa kuhakikisha njia zote zinafunguliwa ili kuwezesha wanyamapori wote kuwa huru kuzunguka katika hifadhi zote nchini.
SAM_3282
Mkuu wa mradi huo wa PROTECT Jon Anderson akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa PROTECT  wa dola za kimarekani Milioni 14.5 wa kulinda mazingira,kukuza uhifadhi na utalii nchini hapa
SAM_3274
Mwenyekiti wa jumuiya ya hifadhi ya jamii Randilen   Daniel Loishaye akizungumza katika uzinduzi huo
SAM_3276
Wadau wa wanyamapori wakiwa wanafatilia hotuba ya Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress
SAM_3311
Balozi  wa Marekani nchini Tanzania Mark Childress akiwa anapunga mikono ishara ya kuagana na wadau mbalimbali waliofika katika uzinduzi huo
SAM_3256
Wanyama aina ya Twiga wakiwa wanapamba hifadhi ya Tarangire
Na Pamela Mollel,Arusha

Serikali ya Marekani kwa kupitia shirika la ushirikiano wa kimataifa
{USAID} imezindua rasmi mradi wa miaka mitano wa kulinda mazingira na
kukuza uhifadhi wa utalii wa  dolla za kimarekani milioni14.5 hapa
nchini ujulikanao kama PROTECT=PROJECT

Uzinduzi huu ambao umefanyika ndani ya eneo la hifadhi ya wanyamapori
linalosimamiwa na jumuiya ya uhifadhi ya wanyamapori {WMA} la Randilen
linalopakana na hifadhi ya taifa tarangire Wilayani Monduli mkoani
Arusha, balozi  wa marekani nchini Tanzania mark Childress amesema
mradi huu unalenga kujenga uwezo wa uhifadhi na kukabiliana na
ujangili na usafirishaji haramu wa wanyamapori nchini kote Tanzania.

Balozi Mark amesema mradi wa PROTECT utalenga kutoa ufumbuzi wa muda
mfupi kwa tatizo kubwa lililopo sasa la ujangili huku likiweka misingi
ya mafanikioya muda mrefu katika vita dhidi ya ujangili sanjari na
kuhimiza ushirikiano kati ya jumuiya za kiraia.

Amesema mradi huu  pia utatoa ruzuku ya miaka mitano ya dolla za
kimarekanio 2.75 milioni kwa jamii inayozunguka hifadhi kwa lengo la
kuwajengea uwezo wa kusimamia raslimali hizo.

Aidha balozi ametangaza mradi mpya wa dola 14 milioni za kimarekani
unaotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni utakaoshughulikia maeneo ya
bayoanuai zilizopo katika hatari ya kutoweka katika ukanda wa
kaskazini mwa Tanzania utakao fahamika kama Endangered Ecosystems
Northern Tanzania project kwa lengo la kupambana na ujangili.kutoa
msaada ya moja kwa moja kwa MWA ,jamii na wadau katika sekta ya utalii
ili kuboresha usimamizi wa wanyamapori.

Kwa upande wa Waziri wa Mali Asili na Utalii Lazaro Nyalandu baada ya
uzinduzi na kusaini mkataba amesema kumekuwa na uvamizi mkubwa katika
maeneo ya hifadhi za taifa na kusema kuna mpango makakati wa
kuhakikisha njia zote zinafunguliwa ili kuwezesha wanyamapori wote
kuwa huru kuzunguka katika hifadhi zote nchini.

Pia amewataka wana jamii wa maeneo ya hifadhi ya jumuiya ya WMA
Randilen kukaa na uongozi wa hifadhi na kutatua changamoto zilizopo.

    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa