Arusha
Home » » ZAMZAM WAIBUKA MABINGWA KOMBE LA NG”OMBE JIJINI ARUSHA‏

ZAMZAM WAIBUKA MABINGWA KOMBE LA NG”OMBE JIJINI ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAM_2918
Mfadhili wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akimkabidhi zawadi ya ng"ombe kocha wa klabu ya Zamzam,Omary Athuman mara baada ya timu yake kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 jana katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_2889
Wachezaji wakiwa wanapambana uwanjani
SAM_2916
Mfadhili wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akimkabidhi zawadi ya Jezi kocha wa klabu ya Zamzam,Omary Athuman mara baada ya timu yake kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 jana katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
SAM_2922
Mashabiki wakiwa wa timu ya Zamzam wakiwa wanashuhudia zawadi ya ng'ombe baada ya timu yao kushinda kwa mabao 2-0
SAM_2902
Mfadhili wa fainali za kombe la Ng"ombe jijini Arusha,Kim Fute akiwa anazungumza mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi
SAM_2874
Umati mkubwa wa mashabiki wa timu ya Zamzam na Nyota wakifatilia mpambano
SAM_2897
Mashabiki mbalimbali wakiwa katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha wakishuhudia mchezo wa fainali baina ya Nyota na Zamzam zilizokutana katika uwanja huo jana,Zamzam waliibuka mabingwa baada ya kuilaza Nyota kwa mabao 2-0
SAM_2895
Mratibu wa mashindano hayo Sanare Mollel akizungumza na wanahabari kuhusu mechi hiyo iliyokuwa ikifanyika katika uwanja wa shule ya Sinoni jijini Arusha
SAM_2877
Taswira katika uwanja huo wa shule ya Sinoni jijini Arusha
SAM_2874Umati mkubwa wa watu katika uwanja wa sinoni wakifatilia mechi kwa ukaribu
SAM_2614Mashabiki wa klabu ya Zamzam wakimyanyua mlinda mlango wa klabu hiyo mara baada ya timu yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa fainali ya kombe la Ng"ombe baada ya kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0 juzi katika uwanja wa shule ya msingi Sinoni jijini Arusha
SAM_2881
Kushoto ni mdau mkubwa wa mtandao wa kijamii wa Jamiiblog Muhamed Akonaay  akiwa na mmiliki wa mtandao huo Pamela Mollel katika uwanja wa sinoni

Klabu ya Zamzam yenye maskani yake Sinoni jijini Arusha juzi wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la Ng”ombe mara baada ya kuilaza klabu ya Nyota kwa jumla ya mabao 2-0.

Kwa ushindi huo Zamzam walikabidhiwa zawadi ya ng”ombe na jezi huku Nyota wakiambulia zawadi ya seti moja ya jezi kama mshindi wa pili katika fainali iliyopigwa katika uwanja wa shule ya msingi ya Sinoni jijini Arusha.

Katika mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa na mbwebwe za kila aina kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu yoyote kuona lango la mwenzake huku mlinda mlango wa Zamzam,Seleman Msuya maarufu kama “Casillas”akionekana kung”ara katika mchezo huo.

Kipindi cha pili kilipowadia klabu ya Zamzam ilifanikiwa kupata mabao kupitia kwa wachezaji wake  Jaff Mbunda dakika ya 50 na Juma Mgunya dakika ya 82 na kupelekea shangwe kwa klabu hiyo.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo,mfadhili wa ligi hiyo,Kim Fute ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya East Link Tz Ltd alisema kuwa lengo kuu la kudhamini fainali hizo ni kuibua vipaji na kusisitiza pia michezo inaondoa tofauti za kidini,kisiasa,kikabila na kuleta umoja.

Naye,mratibu wa michuano hiyo,Richard Mollel alisema kuwa jumla ya timu 12 katika kata mbalimbali za halmashauri ya jiji la Arusha huku lengo lake likiwa ni kuibua vipaji na kuleta umoja ndani ya jamii.

    

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa