Arusha
Home » » WATANZANIA WANAOFANYAKAZI EAC WAADHIMISHI MUUNGANO HOSPITALI YA WILAYA YA MERU

WATANZANIA WANAOFANYAKAZI EAC WAADHIMISHI MUUNGANO HOSPITALI YA WILAYA YA MERU

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Umoja wa Watanzania wanaofanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(WATJAM)yenye makao yake makuu jijini Arusha wakiwasili kwenye hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru kufanya usafi na kutoa misaada mbalimbali kwaajili ya kuadhimisha Siku kuu ya Muungano wa Tanzania leo.
Watanzania wanaofanyakazi kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)yenye makao yake makuu jijini Arusha wakifanya usafi kuzunguka mazingira ya hospitali hiyo leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mganga Mkuu wa hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru,Arusha,Dk Azizi Msuya(kushoto)akipokea sehemu ya zawadi zilizotolewa na Wafanyakazi wa EAC ambao ni Watanzania kutoka kwa Mwenyekiti wa umoja huo,James Kuleiye yenye thamani ya Sh.3.7 milioni.

Na Mwandishi Wetu

Umoja wa Watanzania wanaofanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(WATJAM)yenye makao yake makuu jijini Arusha katika kuhadhimisha Sikukuu ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar leo wametembelea hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Meru kufanya usafi na kutoa misaada mbalimbali yenye thamani ya zaidi ya Shilingi 3.7 milioni

Mwenyekiti wa umoja huo,James Kuleiye amesema wao kama watanzania wameona waitumie siku ya leo kufanya shughuli za kijamii na kuwa karibu na taasisi hiyo kwa lengo kujenga mahusiano mema.

Misaada iliyotolewa ni Maji maluumu ya wagonjwa ,Mashuka 50,Vifaa tiba vya kupima mapigo ya moyo(Presha) na vifaa mbalimbali vya usafi.

Mganga Mkuu wa hospitali hiyo,Aziz Msuya ameshukuru umoja huo kwa moyo wa uzalendo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo licha ya kueleza changamoto inayoikabili hospitali hiyo ya kutokuwa na Wodi ya kuwalaza wagonjwa waliofanyiwa Upasuaji.

Amesema vifaa hivyo vitakua msaada mkubwa kuboresha afya ya mama na mtoto kwani kila mwezi jumla ya wanawake 300 hujifungua huku 50 wakijifungua kwa upasuaji.


Kwa hisani ya Michuzi Media

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa