Home » » NIKKI WA PILI: MIKAKATI NI MINGI BAADA YA PHD

NIKKI WA PILI: MIKAKATI NI MINGI BAADA YA PHD

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Nikki wa Pili 
Rapa Nikki wa Pili kutoka Kampuni ya Weusi ameweka wazi mikakati yake na kile atakachofanya baada ya kumaliza Shahada yake ya Uzamuvu (PhD).
Hivi karibuni Nikki wa Pili ambaye jina lake halisi ni Nickson Simon alitangaza uamuzi wake wa kusoma PhD na tayari ameanza masomo katika Chuo Kikuu ch Dar es Salaam(UDSM) katika masuala ya maendeleo(Development Studies.
 Kupitia mahojiano yafuatayo, pamoja na mambo mengine Nikki wa Pili anaweka wazi anayotarajia kuyafanya katika muziki wa Bongo Fleva baada ya kumaliza elimu PhD.
Starehe: Kuna uhusiano gani wa elimu na sanaa yako?
Nikki wa Pili: Uhusiano unaweza usionekane moja kwa moja, lakini elimu inaweza kunisaidia kwa mambo mengi katika safariyangu ya muziki na maisha nje ya muziki.
Starehe: Mpaka sasa kuna mchango gani uliotoa kutumia elimu yako katika kuendeleza moto za Bongo Fleva?
Nikki wa Pili: Nimejaribu kufanya kwa kiwango fulani katika ushawishi. Kwanza, nimeshiriki harakati za kuishawishi Serikali itambue kikatiba umuhimu wa sekta ya sanaa.
Pili, nimeshiriki nikiwa mstari wa mbele kama mfano, kupinga unyonyaji unaofanywa kupitia milio ya simu. Nilitangaza kujiondoa Kampuni ya Spice VAS Africa na Push Mobile mwaka jana na  baadhi wakafuata baada ya kuelimisha kuhusu unyonyaji huo.
Wasanii wengi bado hawafahamu hata makadirio ya faida au mapato yanayoingia kupitia milio ya nyimbo zao.
Hiyo ni hatari sana. Kampuni za simu zinachukua asilimia 60, mzalishaji anachukua 31 na mpaka hatua ya mwisho msanii anapata asilimia 2 hadi 6.
Harakati za kujiondoa huko zinaathiriwa na mfumo, inahitaji safari ndefu ya ushiriki wa Serikali na uamuzi wa wasanii wenyewe. Kwa hivyo, nikimaliza PhD nitakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuendeleza harakati hizo, ili siku moja tuone muziki wetu unaondolewa mizizi ya unyonyaji.
Mbali na harakati hizo, nimekuwa muelimishaji wa fursa za ajira kupitia semina iliyoandaliwa na Clouds Media Group.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa