Na Beatrice Lyimo, Maelezo-DSM.
WAZIRI
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt. Shukuru Kawambwa (pichani)
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Harambee ya kuchangia kuchangia
ujenzi wa nyumba za walimu vyumba vya madarasa na ununuzi wa samani
katika shule ya Sekondari ya Enaboishu iliyopo mkoani Arusha.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Bw. Emmanuel Munga
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi jijini Dar Es Salaam.
Munga
amesema kuwa Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika siku ya tarehe 25
Oktoba mwaka huu katika shule hiyo wilayani Aremure mkoani Arusha ambapo
Kauli mbiu ya harambee hiyo ni ‘penye nia pana njia’.
Alisema
kuwa, katika harambee hiyo wamewashirikisha wanafunzi wote waliosoma
katika shule hiyo wakiwemo wazazi, viongozi mbali mbali wa Serikali,
Vyama vya siasa, Mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau, shule za jirani
na wananchi kwa ujumla
“katika
harambee hii tunatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 na
fedha zitakazopatikana zitatumika kutatua changamoto zinazozikabili
shule”, alisisitiza Munga
Akizungumzia
kuhusu changamoto zinazoikabili shule hiyo alisema kuwa, shule hiyo
yenye mchanganyiko wa wanafunzi wa kike na wakiume iliyoanza mwaka 1966
inakabiliwa na changamoto za nyumba za walimu, nyumba za madarasa,
mabweni ya wanafunzi na maabara.
Ameongeza
kuwa shule hiyo imetoa baadhi ya viongozi wakubwa waliopo serikalini
wakiwemo Naibu Waziri wa Tamisemi Mhe. Agrey Mwanri na Naibu Katibu wa
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole
Gabriel.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment