Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MADEREVA wa magari ya abiria wameomba Serikali kufufua kiwanda cha kutengeneza matairi cha General Tyre kilichopo Arusha.
Wamedai kuwa ajali nyingi zinazotokea nchini, zinatokana na matairi yasiyo na ubora, yanayoingizwa nchini kwa njia za panya.
Baadhi ya madereva walitoa ushauri huo juzi kwenye maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani, yanayoendelea jijini hapa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu Umoja wa Waendesha Magari aina ya Noah, Elisha Mollel alisema matairi hayo si imara na ndiyo maana yanapasuka mara kwa mara.
Mwakilishi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ambaye ni Ofisa Viwango, Yona Afrika alisema shirika hilo litaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa barabara juu ya kuzingatia ununuzi wa bidhaa bora.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga aliwataka madereva kuacha kuendesha magari kwa mwendo kasi.
Chanzo:Habari Leo
0 comments:
Post a Comment