Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WANACHAMA
wa vikundi vya kuweka na kukopa (VIKOBA) mkoani Arusha wametakiwa
kupanga na kutumia vizuri fedha wanazokusanya ili ziwasaidie kutoka
daraja moja hadi jingine katika maisha yao.
Kauli hiyo ilitolewa mkoani hapa na Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa
Arusha Namelok Sokoine alipoendesha harambee ya utunishaji wa fedha kwa
umoja wa wanavikoba wa Engutoto yenye vikundi 20 na wanachama 600.
Katika utunishaji huo, Namelok alichangia sh milioni 10 huku sh
milioni 12 ikipatikana katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa na viongozi
wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) wilayani Monduli.
“Wanawake nawaomba muendelee kujitokeza na kujiunga katika vikoba
kwani huku ndipo tutaweza kuwa na sauti ya kujitegemea kimapato.
“Lakini pia naomba niwakumbushe jambo muhimu hizi fedha tunazokusanya
nawaomba muonyeshe mfano wa kuzitumia vizuri ili kesho zitusaidie
kutoka daraja moja kwenda jingine kiuchumi,” alisema Namelok.
Naye Katibu wa UWT Engutoto Glory Emmanuel alisema “Tunaomba suala la
ofisi za vikoba uliangalie kwani vikundi havina ofisini. Wanachama
wengi hawana elimu hali inayosababisha kukopa na kutumia fedha vibaya,”
alisema Glory.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment