Na Bertha Mollel - Arusha
Kampuni ya shamba la kuku la Tanzania poultry farm
wameboresha zawadi za washindi wa mashindano ya TPF challenge cup
yanayoendelea kutimua vumbi wailayani Arumeru mkoani Arusha.
Wakurugenzi wa Tanzania poutry farm Amini Bathawab na
msaididizi wake Abdallah Bathawabu walifikia hatua ya kuongeza zawadi
zaidi kwa mchezaji bora, mfungaji bora na golikipa bora baada ya
kuridhishwa na viwango vya ubora wa mashindano hayo ya mpira wa miguu
yaliyofikia hatua ya nusu fainali sasa.
Kwa mujibu wa bathawab wao kama wadhamini wakuu wa
mashindano hayo watatoa kikombe kwa kila mchezaji bora, mfungaji bora
pamoja na golikipa bora sanjari na fedha taslimu kiasi cha shilingi elfu
hamsini ikiwa ni kunogesha ushindani na nidhamu katika mashindano hayo
iweze kuleta malengo yaliyotarajiwa ya kukuza vipaji.
‘’Kama unavyofahamu awali tulipanga kutoa zawadi kwa
mshindi wa kwanza hadi watatu pamoja na timu yenye nidhamu lakini baada
ya kuona ushindani na ubora wa mashindano tumeongeza zawadi hizi ili
kuleta tija kwa wanamichezo wanaoshiriki katika mashindano haya’’
alisema bathawabu.
Mashindano ya TPF chalenge cup yalianza wiki mbili
yakishirikisha jumla ya timu nane na sasa zimebaki timu nne ambazo
zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu zitakazochezwa mwishoni mwa wiki hii.
Mratibu wa mashindano hayo Ahmed shabiby amezitaja timu
zilizoingia nusu fainali kuwa ni TPF SC na Makumira kutoka kundi A na
Chacky accdemy na Imbaseni Accademy kutoka kundi.
Ratiba ya nusu fainali itakuwa inaonyesha nusu fainali ya
kwanza itakuwa kati ya Chacky Accademy dhidi ya Makumira na Imbaseni
Accademy itakutana na TPF na washindi watacheza fainali siku ya
jumapili.
0 comments:
Post a Comment