Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema),
Godbless Lema amedai uwezo wa Serikali kufikiri umefikia kikomo kutokana
na kuweka alama za hatari maeneo ambayo yanaweza kutumika kuliingizia
taifa fedha, huku ikiyaacha bila kuyaendeleza.
Akizungumza wakati akichangia mjadala wa Bajeti
Kuu ya Serikali mwaka 2014/15, Lema alitoa mfano wa eneo la wazi
lililopo mkoani Singida kwamba licha ya kuwa na upepo mkali unaoweza
kuzalisha umeme, Serikali imeweka kibao kikielekeza magari yaende
polepole kutokana na eneo hilo kuwa na upepo mkali.
Alisema mikoa ya Kanda ya Kati ni mikame kutokana
na kuwa na kipindi kirefu cha jua kali kuliko mvua, lakini Serikali
imeshindwa kuweka mitambo ya kuzalisha umeme wa jua.
“Nchi hii sijui tunakwenda wapi, Singida kuna
upepo mkali ambao ungeweza kuzalisha umeme, sasa Serikali haijaweza
kufanya hivyo.” alisema.
Alisema kuwa umeme unaozalishwa na nguvu ya jua
(solar) unaweza kupatikana kwa akiwango kikubwa katika mikoa ya Kanda ya
Kati, lakini licha ya Serikali kulitambua hilo imeshindwa kuzalisha
umeme huo.
“Ndiyo maana niliwahi kusema kuwa Serikali hii
imefikia mwisho wa kufikiri, ukitaka kuamini hilo tizama katika vyanzo
vya mapato, kila mwaka ni vilevile vya soda, bia, sigara na pombe kali”
alisema
Mbunge huyo aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa
inazingatia ushauri inaopewa na watu wa kada mbalimbali, kuachana na
tabia ya kuogopa kusaidia jimbo fulani kwasababu tu linaongozwa na
mbunge wa upinzani.
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment