Namba zimeanza kutolewa kwa washiriki wa mbio za Sokoine
Mini Marathon Km 21 na Km 2 ambazo zitatimua vumbi Aprili 12, 2014 Monduli
mkoani Arusha, rais Jakaya Kikwete ndiye atakayepuliza kipenga cha kuanza mbio
hizo.
Ada ya namba ni Tsh: 2,000 tu, namba zinapatikana Arusha
pale Uwanja wa kumbukumbu ya SHEIKH AMRI ABED KARUME na Monduli pia.
Kwa washiriki wote nje ya mkoa wa Arusha wasiliana na VICTOR
MACHOTA kwa 0787415864 ambaye atapokea usajili kwa njia ya simu na namba yako
utajulishwa kwa SMS na itahifadhiwa hadi utakapoichukua. Mwisho wa kuchukua
namba yako ni Ijumaa April 11, 2014 Arusha mjini.
Kwa wale watakaosajili kwa njia ya simu tunaomba mtume hela
kwa AIRTEL MANEY kwa namba ya Victor Machota, unaombwa uongezee gharama kidogo
ya kutoa pesa mtandaoni.
Kwa wale watakaosajili namba papo kwa papo wawasiliane na
PHAUSTIN BAHA 0753860668 kwa maelezo zaidi na kwa wale wa Monduli wawasiliane
na ROBERT MOLEL kwa 0753739128.
Kwa ratiba kamili hapo baadae pitia blogu zifuatazo; WOTE
MNAKARIBISHWA KUSHIRIKI NA RAIS WA JAMHURI YA TANZANIA.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment