Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA cha Waongoza Watalii Tanzania (TATO) kimetoa msaada wa
pikipiki 15 kwa Jeshi la Polisi mkoani Arusha ikiwa ni sehemu ya kuunga
mkono jitihada za jeshi hilo kupambana na wahalifu hasa wanaotumia
pikipiki ambao wameshamiri katika maeneo mengi nchini.
Akizungumza katika makabidhiano ya pikipiki hizo hivi karibuni,
Mwenyekiti wa Tato, Wilbard George, alisema msaada huo unaweza kuongeza
tija ya Jeshi la Polisi katika kupambana na vitendo vya uhalifu katika
Mkoa wa Arusha ambao ni kitovu cha utalii na kuongeza pato la mkoa.
Alisema chama hicho kimeamua kujitolea kutambua changamoto za vifaa
zinazolikabili jeshi hilo katika kutimiza wajibu wake wa kulinda raia
na mali zao.
Chanzo;tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment