Magoto alisema wapagazi kwa kauli moja wamekubaliana ifikapo Machi 6
mwaka huu, utakuwa mwisho wa kupokea chini ya Sh15,000 au Dola 10 za
Marekani kwa siku na kwamba, ifikapo Machi 7 watagoma
Wapagazi wa Mlima Kilimanjaro na Meru, wametoa siku 30 kwa
kampuni zinazopokea watalii wanaopanda milima hiyo kuanza kuwalipa
Sh15,000 kwa siku, vinginevyo watagoma.
Wapagazi hao ambao hufanya kazi ya kubeba mizigo
ya watalii wanaopanda milima hiyo, walifikia maazimio ya kutangaza mgomo
huo kwenye mikutano ya Chama cha Wapagazi Tanzania (TPO), ambayo
ilifanyika Arusha na Kilimanjaro, jana.
Katibu Mkuu wa TPO, Mugabo Magoto alitangaza maazimio hayo jana baada ya mkutano wa wapagazi uliofanyika mjini Moshi.
Magoto alisema wapagazi kwa kauli moja
wamekubaliana ifikapo Machi 6 mwaka huu, utakuwa mwisho wa kupokea chini
ya Sh15,000 au Dola 10 za Marekani kwa siku na kwamba, ifikapo Machi 7
watagoma.
Mugabo alisema wanataka kulipwa kiwango hicho kwa sababu ndicho kilitangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii mwaka 2008.
Alisema hadi sasa ni kampuni 18 kati ya zaidi ya
300 nchini, ambazo zimekuwa zikilipa, hivyo kuwafanya wapagazi kufanya
kazi kubwa kwa ujira mdogo.
“Kazi ya kubeba mizigo na kupanda Mlima
Kilimanjaro ni kubwa, kila mtu anajua lakini tunashangaa wenye kampuni
wanaendelea kuwanyonya wapagazi,” alisema Mugabo.
Pia, wameazimia kujiunga na Chama cha Wafanyakazi cha Tanzania Porters Union.
na pia wanachama wote wameazimia kujiunga na mfuko wa Pensheni wa NSSF.
Akizungumza katika mkutano na wapagazi hao, meneja
kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha, Jakton Achieng aliwataka wapagazi hao ,
kujitokeza kujiunga na NSSF ili wanufaike na mafao.
Alisema NSSF licha ya kutoa mafao hayo pia, , watasaidia Saccos ya wapagazi hao, kuweza kujiendesha na hivyo kupata faida.
Katika mkutano huo, wapagazi zaidi ya 200
walijiunga na NSSF mkoa wa Arusha huku wengine zaidi 150 wakijiunga na
mfuko huo mkoa wa Kilimanjaro.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment