Home » , » MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATEMBELEA MRADI WA MAJIKO SANIFU NA KUZURU KABURI LA SOKOINE MONDULI

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL, ATEMBELEA MRADI WA MAJIKO SANIFU NA KUZURU KABURI LA SOKOINE MONDULI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange juu ya kusafisha na kuyafanya maji kuwa salama, wakati alipotembelea sehemu ya karakana hiyo inayotumia umeme wa nguvu za jua (Solor Power Energe) February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Bw. Kisioki Moitiko kuhusu utengenezaji wa majiko hayo, wakati alipotembelea kwenye karakana hiyo February 25-2014.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekua Waziri Mkuu wa awamu ya kwanza Marehemu Edward Moringe Sokoine, wakati alipozuru kijijini kwa marehemu Monduli juu Mkoani Arusha February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka ndani ya moja ya nyumba zinazotumia majiko sanifu wakati alipotembelea katika kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha February 25-2014.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akicheza ngoma ya kimasai na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao February 25-2014.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Dkt. Binilith S. Mahenge, akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani Arusha, ambapo ameambatana na Makamu wa Rais kwenye ziara hiyo.
Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Zakia Bilal, akisalimiana na Wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilayani Monduli Mkoani arusha walipofika kijijini hapo kwa ajili ya kuzungumza na wananchi hao February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea kifimbo kutoka kwa wazee wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha February 25-2014, mara baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la kijiji hicho.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkuu wa karakana ya utengenezaji Majiko Sanifu Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha Prof. Robert V. Lange, February 25-2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa kijiji cha Enguiki Wilaya ya Mondoli Mkoani Arusha baada ya kuwahutubia mkutano wa hadhara February 25-2014. (Picha na OMR)


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa