Home » » WANANCHI WAFUKUZA KAZI UONGOZI WA KIJIJI KWA UBADHILIFU

WANANCHI WAFUKUZA KAZI UONGOZI WA KIJIJI KWA UBADHILIFU

KUSHINDWA kusimamia maendeleo kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ,kumepelekea wananchi wa kijiji cha Manyire kata ya Mlangalini ,wilayani Arumeru kuwavua madarakani viongozi wa kijiji hicho akiwemo mwenyekiti  wa kijiji hicho ,Andrea Mayasa na kuzifunga kwa makufuri ofisi za kijiji kwa tuhuma mbalimbali za ubadhilifu wa mali za kijiji na uuzwaji wa maeneo ya wazi kinyume na utaratibu.


Hatua hiyo ilifikiwa katika mkutano maalumu wa hadhara uliofanyika kijijini hapo na kuhudhuliwa na diwani wa kata hiyo,Mathias Manga ambaye alikubal;iana na  maadhimio ya wanakijiji hao walioafikiana kuwatimua viongozi wao huku wakisisitiza lazima wawafikishe mahakamani.

Kabla ya kufikia hatua ya kuwatimua wananchi hao waliokuwa na jazba kupita kiasi,walimtuhumu mwenyekiti wa kijiji hicho,Adrea Mayasa kushiriki kuuza maeneo ya huduma na fedha kutia mfukoni,ugawaji wa viwanja kiholela,kushindwa kusoma  mapato na matumizi ya kijiji kwa zaidi ya miaka mitatu,na kuwachangisha michango mbalimbali ya fedha bila kupata maelekezo ya matumizi ya fedha hizo.

Awali diwani wa kata hiyo Mathias Manga aliwasihi wananchi hao kuacha jazba na kutowafukuza viongozi wao hadi wafuate taratibu mahususi ikiwemo kumwarifu mkuu wa wilaya hiyo Nyirembe Munasa  juu ya tuhuma za viongozi hao,lakini wananchi hao walikuja juu huku wakipiga kelele wakisema waondoke! waondoke!
hatua ambayo diwani huyo alilazimika kukubaliana nao na kuamuru viongozi hao wasimame hadi hapo uchunguzi wa mkuu wa wilaya hiyo,utakapotolea ufafanuzi sakata hilo.

Diwani Manga alisema viongozi hao walikuwa kiungo muhimu katika shughuli za kuleta maendeleo katika kata hiyo ila kutokana na maamuzi ya wananchi hakuwa na uwezo wa kupingana ispokuwa alibariki maamuzi hayo na kuagiza tuhuma za viongozi hao na maadhimio ya wanakijiji yaandikwe na nakala zipelekwe kwa viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani humo.

Akijibu hoja za wananchi hao mwenyekiti aliyevuliwa madaraka, alisemayeye bado ni mwenyekiti halali na kwamba tuhuma
zinazoelekezwa kwake ni uzushi mtupu ,umbeya na majungu
yanayopandiikizwa na wananchi wanaomchukia na kwamba anachofanya sasa ni kumsubili mkuu wa wilaya hiyo ili amweleze ukweli wa kilichopo ndani ya kijiji hicho na si vinginevyo.


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa