Arusha
Home » » Wakamatwa na madawa ya kulevya

Wakamatwa na madawa ya kulevya

JESHI la Polisi mkoani Arusha limekamata madawa ya kulevya aina ya mirungi kilogramu 30  thamani yake ikiwa bado haijajulikana  ikitokea Namanga kuingia mkoani hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Liberatus Sabas alisema tukio la kukamatwa kwa watuhumiwa hao,lilitokea Decemba 24,mwaka huu majira ya saa saba mchana katika eneo la Ngaramtoni wilayani Arumeru.

Aidha amesema kuwa kukammatwa kwa watuhumiwa hao kunatokana na ushirikiano wa raia wema waliotoa taarifa katika kituo cha polisi Ngaramtoni,ambapo askari awaliokuwa doria walisimamisha gari lenye namba za usajili T703 CMC aina ya Noah iliyokuwa ikiendeshwa na Zakayo Mwita (26) akiwa na mwenzake aitwaye Juma Ramadhani (24).

Hata hivyo amesema madawa hayo yalikuwa yamefichwa kwenye bampa la tairi za mbele na ndani ya kava za milango (side door cover),upande wa dereva na upande wa pili,huku watuhumiwa wakiwa wanasafirisha madawa hayo wakati wakijua ni jambo lililopo kinyume cha sheria.

Amesema wakati wa ukaguzi walibaini kuwepo kwa viroba 30 vya madawa hayo vyenye uzito huo,huku watuhumiwa wakiendelea kuhojiwa na Jeshi hilo mkoani hapa ili kuweza kubaini wahusika wengine ambapo watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa