SERIKALI wilayani Longido imeombwa kuingilia kati haraka mgogoro wa
ardhi baina ya wananchi wa Kijiji cha Kitendeni Kata ya Kamwanga na
mkulima mkubwa mzawa, Boniface Lazaro, kuepusha kuvurugika amani katika
eneo hilo. Rai hiyo ilitolewa juzi kijijini hapo na Diwani wa
Kata hiyo Komolo Simeli na Mtendaji wa Kata hiyo Thomas Maitiyaki kwa
nyakati tofauti.
Wametoa kauli hiuyo baada ya wananchi wa eneo hilo ambao ni Wamasai kutaka kuchoma nyumba ya mwekezaji huyo.
Diwani alisema wananchi wamefikia hatua hiyo ambayo itahatarisha hali ya usalama kijijini hapo nakuvituhumu vyombo vya dola kutokushughulikia migogoro hiyo ya ardhi.
“Leo(juzi) tumejitahidi kama viongozi kuwatuliza hasira vijana hawa ambao walitaka kuchoma nyumba ya mzee huyo na tumejitahidi pia kusuluhisha mgogoro huu.
“Mkulima huyo mkubwa anaonyesha daliliza kupora ardhi hii ya Peria Laiser (mmiliki halali) baada ya kugawiwa na ukoo kutokana na ardhi hii kumilikiwa na ukoo wa Ole Nguliya,’’ alisema Komolo.
Laiser anayedaiwa kuwa mmiliki halali wa eneo hilo alisema kuwa Juni 6 mwaka 1990 familia yao ilimkabidhi Lazaro eneo hilo na kuandikishanamkataba ambao ulionyesha iwapo familia hiyo itahitaji shamba lao, Lazaro atalazimika kuliachia.
“Mwaka 2002 sisi kama familia tulimfuata na kumueleza kuwa tunataka kuendelea kutumia shamba hilo lakini alikataa.
“Tumejitahidi kutumia njia za sheria ikiwa ni pamoja na kupeleka suala hili katika Baraza la Ardhi la kijiji na kushinda lakini suala hilo bado limebaki kuendelea kutopata suluhisho la kudumu kutokana na mzee huyo kuendelea kung’angania shamba,”alisema Laiser.
Akizungumza kwa simu na gazeti hili mlalamikiwa Lazaro alidai kushangazwa na madai hayo kuwa yeye si mmiliki halali wa ardhi hiyo akisisitiza kuwa amekuwa akiitumia ardhi hiyo kwa zaidi ya miaka 40.
Chanzo;Mtanzania
0 comments:
Post a Comment