TAASISI inayohimiza Mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRA), imesema juhudi
za kuleta mapinduzi ya kijani nchini kwa lengo la kuboresha hali ya
upatikanaji wa chakula, zinaanza kuonyesha matunda. Taasisi hiyo ambayo
Mwenyekiti wake ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN),
Kofi Annan, matunda hayo ni baada ya kampuni zinazojishughulisha na
kilimo nchini Tanzania na wadau wengine wa sekta hiyo kuanza kuzalisha
mbegu bora za mahindi, mtama na alizeti.
Akizungumza mjini hapa jana, Ofisa wa AGRA anayeshughulika na Programu ya Mfumo wa Mbegu Afrika (PASS), Dk. George Bigirwa, alisema kupatikana kwa mbegu bora ni muhimu kufikia ndoto ya mapinduzi ya kijani.
“Ongezeko la ubora wa mbegu na ufanisi wake ni kitu muhimu katika kuhakikisha usalama wa chakula na kufikia mapinduzi ya kijani,” alisema Dk. Bigirwa.
Alisema kwa msaada wa AGRA, kampuni 11 za Tanzania zimepiga hatua kubwa katika uzalishaji wa mbegu bora na zenye ufanisi mkubwa shambani.
Alisema kati ya kampuni 11 yaliyofaidika na msaada wa kifedha na ujengaji uwezo wa AGRA bado kampuni nane zinaendelea kusaidiwa.
Aidha, alisema kampuni tatu zinajiendesha zenyewe na AGRA wanachofanya ni kuhakikisha kwamba yanaendelea kutoa ushauri inapobidi juu ya kuendelea kuboresha shughuli zao hasa eneo la masoko, sera na kuendesha mafunzo mafupi na ya muda mrefu.
Alisema kuanzia mwaka 2007, AGRA imeshatumia zaidi ya Dola 11,084,733 za Marekani kusaidia mradi wa mbegu chini ya PASS.
Aliitaja baadhi ya misaada hiyo katika miradi 36 imetolewa katika mfumo wa mitaji na ruzuku kwa kampuni ya mbegu.
Alikiri kwamba kuwa na mashamba makubwa ya mbegu, kunatoa fursa kwa wakulima wengi kupata mbegu zilizofanyiwa utafiti, kuthibitishwa ubora wake huku wakizipata kwa bei nafuu.
Aidha, alisema kwa kuzalisha mbegu bora nchini, Taifa linaokoa fedha za kigeni ambazo hutumika kununulia mbegu kutoka nje.
Alisema kukosena kwa mbegu bora na zenye ufanisi shambani kumekuwa kikwazo kwa Tanzania kama yalivyo mataifa mengine ya Afrika yanayopigana kuwa na uzalishaji wa kutosha wa chakula.
Alisema kutokana na mazingira hayo, PASS imelenga kuhakikisha wakulima wanakuwa na mbegu bora zenye ufanisi shambani kwa lengo la kuongeza tija na kuwa na chakula cha kutosha na hivyo kubadili maisha ya wakulima.
Alisema PASS inasaidia makundi ya wanaozalisha mbegu ambao hufanya kazi kwa karibu na wakulima kupata aina mpya ya mbegu zenye ubora wa hali ya juu na zenye tija inayotakiwa.
Mafanikio yakishapatikana katika utafutaji wa mbegu bora kwa kusaidiana na wakulima, programu ya PASS hutoa fedha za mafunzo kwa wajasirimali ambao huanzisha makampuni ya mbegu na kwa kutumia mashamba yao huzalisha na kusambaza mbegu hizo.
Mkulima mmoja wa Babati, Rajesh Atiya wa Kampuni ya Mbegu ya Krishna Seed Ltd, aliwaambia maofisa wa AGRA kuwa kutokana na msaada wa elimu na mtaji aliowezeshwa atakuwa na mavuno makubwa.
Alisema AGRA ilimsaidia kukutana na wakulima wengine na mawakala wa mbegu na hivyo kumfanya ajue zaidi masuala ya kilimo.
Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Suba Agro Trading & Engineering Ltd, Sarah Muya, alisema tangu aanze kupata msaada wa AGRA mwaka 2012, tija imekuwa ikiongezeka.
Alisema PASS huendeshwa kwa kuoanisha programu ndogo nne zinazoleta mnyororo wa thamani katika utafiti, uzalishaji wa mbegu bora na tija mashambani.
Alisema programu hiyo huanza kwa kutoa mafunzo kwa wazalishaji wapya wa mbegu na wataalamu na kumalizikia kwa kufikisha mbegu bora kwa mkulima kupitia mawakala wa pembejeo waliopo vijijini.
HABARI KWA HISANI YA GAZETI LA MTANZANIA

0 comments:
Post a Comment