Arusha
Home » » MTUHUMIWA WA UGAIDI WA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KANISANI JIJINI ARUSHA AKABIDHIWA HATI YA MSHTAKA

MTUHUMIWA WA UGAIDI WA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA KANISANI JIJINI ARUSHA AKABIDHIWA HATI YA MSHTAKA






Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Arumeru, Devotha
 Kamuzora jana alimkabidhi  hati ya mashitaka yanayomkabili, 
Victor Ambrose (20) ambaye ni mtuhumiwa pekee aliyepandishwa
 kizimbani  baada ya kutokea  shambulio la bomu katika Kanisa 
la Mtakatifu  Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini Arusha.
Ambrose alikabidhiwa hati hiyo ya mashitaka yanayomkabili
 jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arumeru jijini Arusha
 na kuambiwa na wakili wa Serikali, Adelaide  Kasala  kuwa 
upelelezi dhidi ya kesi hiyo, haujakamilika na kumuomba 
Hakimu Kamuzora  kutaja tarehe nyingine.
Hakimu Kamuzora kabla ya kuahirisha kesi hiyo alimuuliza 
Ambrose kama alipewa hati yake dhidi ya mshitaka yanayomkabili. 
Ambrose alipojibu, “hapana.” Baada ya jibu hilo,

Hakimu alitoa hati hiyo na Ambrose kukabidhiwa na
 kuahirisha kesi hiyo hadi Juni 24.Ambrose ambaye ni 
dereva wa bodaboda na mkazi wa Mrombo jijini Arusha,
 mara ya kwanza alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
 jijini Arusha na baadaye kuhamishiwa Mahakama ya Wilaya
 ya Arumeru na kusomewa mashitaka yake kwa mara ya tatu
 sasa huku akitakiwa kutojibu lolote, kutokana na  Mahakama 
hiyo kutokuwa na uwezo kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.

Wakili wa Serikali, Adelaide Kasala  alidai mahakamani hapo 
Victor alitenda makosa hayo Mei 5, mwaka huu katika Kanisa 
la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti jijini.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa