Home » » KANISA LA SAFINA JIJINI ARUSHA LAFANYA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA TOBA

KANISA LA SAFINA JIJINI ARUSHA LAFANYA MAOMBI YA KULIOMBEA TAIFA TOBA


Na UWESU

Watanzania wameaswa kumrudia mungu na kumuomba toba kwa ajili ya kuikomboa nchi kuondokana na magonjwa, umasikini na majanga mbalimbali.
Hayo yamesemwa ndani ya uwaja huu wa Sheikh Amri Abeid ambamo waumini wa kanisa la Safina jijini hapa wamekusanyika kufanya toba kwa ajili ya taifa la Tanzania kuliombea taifa hili kwa mwenyezi Mungu alijalie amani na kuliondolea kila aina ya majanga, huku wakiwa katika sare maalum ya magunia kuonyesha unyenyekevu mbele ya Mungu
Muhubiri Jovin Msuya akihutubia kwenye maombi hayo amesema matatizo yanayoikumba nchi yetu hivi sasa hayatakwisha kama watanzania hawatamamrudia mwenyezi Mungu na kuomba toba ya kweli. Amesema pamoja na kutubu huko watanzania hawana budi kutafuta chanzo cha matatizo yao hali itakayowafanya kujua wapi walipoteleza na kupelekea nchi kuwa hapa ilipo hivi sasa.
Nao baadhi ya waumini wa dhehebu hilo wamesema wameamua kufanya toba hiyo kumuomba Mungu alijalie taifa hili kutokana na matatizo lukuki ikiwemo umasikini uliokithiri miongoni mwa watanzania wengi licha ya nchi kubarikiwa rasilimali nyingi kama vile madini na vivutio vingi vya utalii.

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa