Home » » MKUTANO WA 16 WA KAMATI YA VIWANGO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

MKUTANO WA 16 WA KAMATI YA VIWANGO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Leandri Kinabo, Kaimu mkurugenzi TBS, akioingea na waandishi wa habari
 Dr. Enos Bukuku, Mgeni Rasmi
Wajumbe wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini
***************
Na Idd Uwesu( Arusha Yetu blog)
Mkutano wa 16 wa kamati ya viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki umeanza jijini Arusha ukiwaahusisha wakuu wa mashirika ya viwango ya nchi wanachama wa umoja huo.
Mkutano huo wenye lengo la kujadili masuala mbalimbali yahusuyo ubora wa bidhaa zinazosambazwa na wafanyabiashara katika soko la nchi wanachama pia unatarajiwa kujadili suala la mafuta ambalo limekuwa na utata kwa kipindi kirefu kutokana na nchi hizo kuwa na viwango tofauti
Mgeni rasmi katika ufunguzi huo Dr. Enos Bukuku ambaye ni Naibu katibu Mkuu wa Mipango na Miundombinu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aliufungua rasmi mkutano huo na kuwataka wajumbe hao kuutumia mkutano kujadili kwa kina mambo muhimu kuhusu viwango vya ubora wa bidhaa  ili kuwawezesha wana afrika Mashariki kufanya vizuri hata kwenye masoko ya nje huku akitolea mfano soko AGOA
Kwa upande wao wakuu wa Mashirika ya viwango ya Tanzania na Kenya  Leandri Kinabo, Kaimu mkurugenzi TBS na Eva Oduor, Mkurugenzi KBS wamesema mkutano huo utajadili mambo mengi huku kipaumbele kikipewa kwa suala la Mafuta ambapo nchi wanachama wanatumia mafuta hayo kwa viwango tofauti na hivyo kuwa na hali ya kutofautiana bidhaa hiyo inapofika sokoni.
Mkutano huo pia unashirikisha wataalamu wa vipimo kutoka mashirika mbalimbali na unasimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa