Mbunge mteule wa Arumeru Mashariki Mh. Joshua Nasari akiongea baada ya kutangazwa kuwa mshindi asubuhi hii huko Arumeru |
Matokeo ya kura za Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki yametangazwa sasa hivi na Msimamizi wa Uchaguzi na Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw Joshua Nassari kuwa mshindi baada ya kupata kura 32,972 dhidi ya mpinzani wake wa karibu kutoka CCM Bw Sioi Sumari aliyepata kura 26,757
Matokeo kwa Vyama vingine sita vilivyoshiriki ni kama ifuatavyo
DP -77
NRA - 35
AFP - 139
UPDB - 18
TLP - 18
SAU - 22
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na aliojitokeza na kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
Wakati huo huo, habari kutoka Mwanza zinasema CHADEMA kimeshinda katika uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kirumba mkoani Mwanza.
Msimamizi wa uchaguzi huo, Bw. Aloyce Mkono, amemtangaza kuwa mshindi mgombea wa Chadema Mh Dany Kahungu kwa kura 2,938 dhidi ya mgombea wa CCM Mh Jackson Masamaki aaliyepata kura 2,131.
Wagombea wengine walioshindwa vibaya katika uchaguzi ni pamoja na Mh Haji Issa wa CUF aliyepata kura 184, Mh Kasala Muhana wa UDP amepata kura 7 na Mh Athuman Jumanne wa NCCR Mageuzi aliyeambulia 0 katika uchaguzi huo .
Msimamizi huyo alisema kuwa uchaguzi huo umefanyika katika hali ya amani na utulivu,na kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo na kuonyesha utulivu mkubwa wakati wa uchaguzi na zoezi la kutangazwa kwa matokeo.
Kwa hisani ya Michuzi Blog
1 comments:
Ushindi wa CHADEMA ni wazi kwamba watanzania wengi wakiwakilishwa na wananchi wa arumeru wamechoka kuchezewa akili, wanataka mabadiliko. Vizuri sana, naipongeza CHADEMA, nawapongeza watanzania waliotuwakilisha katika jimbo la Arumeru
Post a Comment