Home » » SAU CHATETA JUU YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA

SAU CHATETA JUU YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA



NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE-ARUSHA

CHAMA cha Sauti ya umma(SAU)kimesema kuwa kinatarajia kushinikiza msajili wa vyama vya siasa hapa nchini Bw John Tendwa kujiuzulu kwa kuwa mpaka sasa Msajili huyo anashindwa kufanya kazi zake za kulea vyama kwa mujibu wa Sheria hali ambayo inasababisha vyama vingi kukosa haki zake za msingi.
Akongea na Waandishi wa habari katika jimbo la Arumeru Mashariki mapema leo Bw Johnson Mwongosi ambaye ni Katibu mwenezi wa taifa katika chama hicho kutoka katika chama hicho alisema kuwa msajili huyo ameshindwa kufanya kazi zake za msingi za kulea vyama
Bw Mwogosi alibanisha kuwa kwa vyama ambavyo ndio vinachipukia kwa sasa vina kosa haki zake za msingi na badala yake vyama venye majina ndivyo vinavyoangaliwa pekee.
“huyu msamjili kama haya yatendelea ni wazi kuwa tutahakiokisha kuwa anajiuzulu lkwa kuwa halei vyama vidohgo sasa ni bora ajiuzulu na anaonekana hatujsaidii kabisa sasa uhai wa vyama hivi ukio wapi”alihoji Bw Mwagosi
Pia aliongeza kuwa mara nyingi wao wamemtafuta Msajili huyo kwa ajili ya matatizo mbalimbali lakini msajill huyo amekuwa akikwakwepa bila majibu na ufumbuzi wa matatizo.
Akielezea hali ya uchaguzi katika jimbo la Arumeru Mashariki alisema kuwa wamejipangavema kuweza kufanya mapinduzi ya hali ya juu sana ambapo watafanya shugiuli nzima za kampeni kwa njia ya Helikopta
Alifafanua kuwa wao watakuwa na kamepni za tofauti kabisa kwa kuwa wataanza kwenda nyumba kwa nyumba ambapo pia wataweza kufafanua juu ya chama chao na hali ya mafanik8io hata mara baada ya uchaguzi kupita
Habari kwa Hisani ya Full Shangwe Blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa