Home » » MIKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KATA YA SONGORO ARUMERU.

MIKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KATA YA SONGORO ARUMERU.



Vijana wa Sura wakizuia msafara wa mgombea wa CCM Sioi Sumari ili kumsalimia wakati msafara huo ukipita eneo lao kwenda kwenye mkutano wa kampeni.
 Mfugaji katika kata ya Songoro ambaye jina halikupatikana mara moja akishangilia CCM wakati msafara wa mgombea wa chama hicho Sioi Sumari ulipopita katika kata hiyo.
Sioi akihutubia mkutano wa kampeni kijiji cha Sura kata ya Songoro jimbo la Arumeru Mashariki.
Wananchi wa kijiji cha Sura wakishangilia bada ya kukunwa na hotuba ya mgombea wa CCM.

Asiera Jacob mwenye umri wa miaka 78 wa Kijiji cha Sura kata ya Songoro, akifuatilia kwa makini hotuba katika mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea wa CCM Sioi Sumari kwenye kijiji hicho.
Wazee wa Songoro wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgombea wa CCM.
Vijana wakiwa wamepanda mti kumuona mgombea wa CCM Sioi katika mkutano uliofanyika kata ya Songoro.
Kina mama wakimbeba Sioi baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni kijiji cha Mulala  kata ya Songoro jimbo la Arumeru Mashariki.
 Mjumbe wa NEC Oganaizesheni CCM, Asha Abdallah Juma akihutubia mkutano wa kampeni kijiji  cha Sura.
Sioi (watatu kushoto) na mratibu kampeni za CCM jimbo la Arumeru Mashariki Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto)wakitoka kukagua ujenzi wa kituo cha afya cha Mulala Kata ya Songoro jimboni humo baada ya kuahidi kumalizia ujenzi wa kituo hicho katika mkutano wa kampeni.
(Picha zote na Bashir Nkoromo). 

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa