Home » » JK Mgeni rasmi katika mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchini mbalimbali

JK Mgeni rasmi katika mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchini mbalimbali



Na Tiganya Vincent-Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufungua mkutano wa Kimataifa wa Mamlaka za Kuzuia na Kupambana na Rushwa kutoka nchini mbalimbali .
Kauli hiyo imetolewa leo na Msemaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  Doreen Kapwani wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizo mjini Arusha.
Kapwani amesema kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa namna hiyo kufanyika nchini ambapo zaidi ya washiriki 65 kutoka nchi mbalimbali wanatarajia kushiriki mkutano huo wa siku tatu.
Amesema kuwa mkutano huo unatarajia kushirikisha Nchi kama vile Morocco , Uingereza, Qatar, Uganda, Romania, Brazil, Austria, india, Belgium , Spain, Ukraine , Malsiyia , Namibia na Mwenyeji Tanzania.
Kwapwani amesema kuwa mkutano unafanyika hapa nchini wakati Tanzania imepata heshimiwa kubwa ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dk. Edward Hoseah amechaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri juu ya Rushwa ya Umoja wa Afrika Machi mwaka huu

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa