Arusha
Home » » MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO ATOWEKA NYUMBANI

MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO ATOWEKA NYUMBANI

Valentina Ngoya MTOTO, Valentina Ngoya (14), Mkazi wa Songambele, Mererani mkoani Manyara anatafutwa na wazazi wake baada ya kuondoka nyumbani kwao tangu Novemba 3 mwaka huu akienda shule.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, baba mzazi wa mtoto huyo, Ngoya Ogwalo, ambaye ni mkazi wa Busanga wilayani Rorya Mara, alisema kuwa tayari wameshatoa polisi Mirerani Novemba 4 mwaka huu, iliyosajiliwa mir/RB/2077/2014.
Alisema kuwa mtoto huyo ni mwanafunzi wa darasa la tano shule ya Msingi Tanzanite na alikuwa akiishi kwa shemeji yake, Odondo Charles pamoja na familia yake kwa zaidi ya miaka minne sasa.
“Jumanne saa 9:00 alasiri nilipigiwa simu na Charles akiniambia Valentina aliondoka nyumbani toka jana na hajarudi, ila kuna taarifa kuwa alionekana akipanda gari kuelekea Arusha…
“Aliniambia kabla hajaondoka alirudi nyumbani majira ya saa 7:00 mchana akidai amerudishwa nyumbani akachukue fedha za mtihani, ambapo walimpa sh 2,000 kisha akaondoka,” alisema Ogwalo.
Alisema kuwa yeye si mwenyeji jijini Arusha ingawa alifanikiwa kufikishwa kwenye basi alilopanda mtoto wake, ambako dereva wa gari hilo alimweleza kuwa ni kweli kuna mtoto alipanda gari hilo na abiria wakamtilia shaka na wakakubaliana wakifika Arusha wampeleke kituo cha polisi ili aweze kurudishwa kwao, lakini hawakujua alishukia kituo gani.
“Mara ya mwisho niliongea naye Novemba Mosi mwaka huu, akawa anataka kuongea na mama yake ambaye kwa sasa ni mgonjwa, nikamwambia hayupo karibu akataka nimtumie nauli ili aweze kuja nyumbani Musoma kumuona, nikamwambia nitatafuta fedha nimtumie nauli….
“Lakini wakati tukiendelea kuongea yeye akitumia simu ya baba yake mlezi simu ilikatika,  mawasiliano hayakuwa mazuri hivyo sijajua nini kiliendela, hivyo naomba yeyote atakayemuona mtoto huyo atoe taarifa kituo cha polisi,” alisema Ngoya.
Mlezi wa mtoto huyo, Charles akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu, alisema baada ya Valentina kupotea, waliamua kufuatilia shuleni kwao ambako walibaini kuwa hakuwa ametumwa fedha za mtihani kama alivyowaeleza.
Chanzo:Tanzania Daima
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa