Arusha
Home » » NAIBU WAZIRI WA MICHEZO ANASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI KILICHOPO CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA

NAIBU WAZIRI WA MICHEZO ANASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA KITUO CHA UTAMADUNI KILICHOPO CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakicheza ngoma ya Sindimba wakati Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (hayupo pichani) alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) akiwaangalia wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha (hawapo pichani) wakicheza ngoma ya kabila la wa Meru wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Randall Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho kinachojengwa chuoni hapo, watatu kulia ni Afisa Michezo wa Mkoa Mwamvita Okeng’o na wa nne kulia ni Afisa utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiangalia mchoro wa ramani ya Kituo cha Utamaduni kinachojengwa katika chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo. Kulia ni Afisa utamaduni wilaya ya Arumeru Senyael Pallangyo akifuatiwa na Randall Stubbs ambaye ni Meneja Mradi wa kituo hicho.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa Kituo cha Utamaduni kilichopo chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha wakati alipotembelea kituo hicho hivi karibuni kwa ajili ya kuona shughuli za kitamaduni zinazofanyika kituoni hapo.Picha na wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa