Arusha
Home » » KONGAMANO LA SABA LA ELIMU YA JUU LAENDELEA JIJINI ARUSHA‏

KONGAMANO LA SABA LA ELIMU YA JUU LAENDELEA JIJINI ARUSHA‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, Profesa Awadh Mawenya, ambaye ni mgeni rasmi katika kongamano la saba la elimu ya juu linalofanyika jijini Arusha akiongea machache mara baada ya kumaliza kutoa mada. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU), Profesa Yunus Mgaya akiwashukuru washiriki kufika katika kongamano la saba la elimu ya juu linalofanyika jijini Arusha. Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
  Prof. Ephata E. Kaaya, mwenyekiti wa Makamu wakuu wa Vyuo vikuu Tanzania akiongea machache. 
Meza kuu.
Prof. Sylvia Temu, Mkurugenzi - Idara ya Elimu ya Juu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi akiongea na vyombo vya habari juu ya mikakati na mipango ya kongamano la saba la elimu ya juu lililoandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na Tume ya Vyuo Vikuu nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) pamoja na Kamati ya Wakuu wa vyuo Vikuu nchini (CVCPT) likiendana sambamba na maonyesho.
Washiriki wa kongamano la elimu ya juu kutoka katika vyuo na taasisi mbali mbali zinazohusika na masuala ya elimu wakifuatilia mada.
Washiriki wakiwa katika picha za pamoja.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa