Arusha
Home » » PHIDESIA MBUNGE VITI MAALUM AWATAKA WANANCHI WASIRUBUNIWE‏

PHIDESIA MBUNGE VITI MAALUM AWATAKA WANANCHI WASIRUBUNIWE‏

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
SAM_4394Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima aliyeshinda katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).akizungumza katika mkutano wa chama cha mapinduzi jana mtaa wa kati (CCM MKOA)wakati wagombea 12 wa chama hicho walipofanya ziara ya kutembelea kila kata na kujinadi kwa wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho ambapo aliwataka wananchi wasirubuniwe na kama walipewa rushwa na mgombea yeyote wasimchague bali wamchague kiongozi sahihi wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  katika jimbo la Arusha(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
SAM_4366Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalimaambaye alishinda katika  kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A",Mkurugenzi wa Phide entertainment akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Monaban yajijini Arusha,Philemon Mollel ambaye pia ni Mgombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM katika ofisi za (CCM Mkoa) jijini Arusha jana
SAM_4398Katibu wa wazazi Mkoa wa Arusha Mayasa Kimbau akizungumza katika mkutano wa kuwanadi wagombea Ubunge kupitia chama cha mapinduzi mtaa wa kati jijini Arusha ambapo aliwataka wapambe wawagombea watulize mung'ari zao na kuacha tabia ya kukebihana huku akisisitiza wananchi kuchagua kiongozi bora
SAM_4363Kada maarufu wa chama cha mapinduzi ambaye pia  ni mfanyabiashara wa madini jijini Arusha Justine Nyari, anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge akiteta jambo na Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment kabla ya mkutano wao wa kujinadi kuanza
SAM_4368Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment akibadilishana mawazo na wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge
SAM_4374Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" na Mkurugenzi wa Phide entertainment akiwa katika picha ya pamoja na watia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM
SAM_4376Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A"na Mkurugenzi wa Phide entertainment, akisalimiana na mtia nia nafasi ya Ubunge kupitia chama cha mapinduzi CCM Thomas Munisi ,ambapo Mwakitalima aliibuka  mshindi katika kura za maoni za kutafuta wabunge wa viti maalum mkoa wa Arusha kupitia jumuiya ya wazazi wa chama cha Mapinduzi ( CCM ).
SAM_4372Mbunge viti maalum Wazazi Phidesia Mwakitalima  ambaye pia ni Afisa masoko wa Triple "A" akisalimiana na wadau ambao ni watia nia Ubunge na Udiwani,kushoto ni Simba Salum anayeomba chama cha mapinduzi kumpitisha kuwania nafasi ya udiwani mtaa wa kati bondeni na kulia wakili msomi Edimond Ngemela anayeomba ridhaa ya ccm katika nafasi ya ubunge

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa