Arusha
Home » » WAWILI WAKAMATWA NA BUNDUKI

WAWILI WAKAMATWA NA BUNDUKI

 Polisi wilayani Ngorongoro, Mkoa wa Arusha, inawashikilia wafugaji wawili kwa kosa la kukutwa na bunduki aina ya Rifle wanayodaiwa kuitumia kufanya uhalifu wilayani hapa na Kenya.
Katika msako ulioongozwa na Mkuu wa Polisi wa wilaya hiyo, Mrakibu (SP), Ally Mohamed Mkalipa alisema walifanikiwa kukamata silaha hiyo iliyokuwa imefichwa porini karibu na boma la ng’ombe la mfugaji mmoja.
Akizungumza jana na gazeti hili, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Liberatus Sabas aliwataja wafugaji hao kuwa ni wakazi wa Kijiji cha Soitisambu.
Kamanda Sabas alitaja silaha hiyo ni Rifle 370 na tukio hilo lilitokea Januari 10, mwaka huu saa 11 jioni katika Kitongoji cha Silalei, Kijiji cha Soitisambu, Loliondo.
 Chanzo:Mwananchi
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa