Arusha
Home » » ‘WANANCHI KUWENI MAKINI NA KAULI ZA WANASIASA’

‘WANANCHI KUWENI MAKINI NA KAULI ZA WANASIASA’

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

WANANCHI wametakiwa kuwa makini na kauli za wanasiasa, kwani si kila kitu wanachosema ni cha kweli kwa kuwa baadhi yao hupotosha jamii kwa maslahi yao binafsi.
Akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia kwaya ya Patano la Kanisa la KKKT Usharika wa Likamba, wilayani Arumeru, mkoani Arusha mwishoni mwa wiki, Wakili Joseph Makandege, alionya kuwa kauli za upotoshaji katika masuala mbalimbali nchini hususan ya kisheria zinaweza kuleta madhara makubwa kwa taifa.
“Kama mwanasheria, ningependa kuwashauri wanasiasa wetu kuacha kuingilia mashauri yaliyopo mahakamani au ambayo yameamuliwa na vyombo halali vya kimahakama kwa kutoa kauli ambazo zinawapotosha wananchi.
“Wakiendelea na tabia ya kuhoji uhalali wa maamuzi ya mahakama, itapelekea hata wananchi kutokuwa na imani na mahakama zetu, jambo ambalo linaweza kusababisha haki za watu wanyonge kupotea,” alisema Makandege ambaye pia ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa makapuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP)
Alieleza kauli hizo zinachangia kuiathiri jamii ambayo pengine hawajui ukweli kuhusu jambo linaloongelewa kwa kuwa wengi wao wanaamini kuwa kila kauli ya mwanasiasa ina ukweli.
Mwanasheria huyo ambaye alimwakilisha Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPTL/PAP, Harbinder Singh Sethi, akitolea mfano tuhuma zinazoendelea kuhusu kutwaliwa kwa kampuni ya IPTL na PAP pamoja na fedha za IPTL zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow ya Tegeta (IPTL Tegeta Escrow Account) katika Benki Kuu ya Tanzania, alisema licha ya wanasiasa  kutambua ukweli kwamba akaunti hiyo na fedha zote zilizokuwemo hazikuwa za umma, bado wanaendelea kuiongopea jamii kwamba fedha hizo zilikuwa mali ya umma.
Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa