Home » » MSANII WA FILAMU SAJUKI AANGUKA JUKWAANI ARUSHA

MSANII WA FILAMU SAJUKI AANGUKA JUKWAANI ARUSHA
Sajuki akipumzika kwa muda baada ya kuanguka
Sajuki akinyanyuliwa
Akitelemshwa toka jukwaani

HALI ya msanii wa filamu nchini,Juma Said Kilowoko maarufu kama Sajuki imeelezwa si ya kuridhisha mara baada ya msanii huyo juzi kuanguka jukwaani kwa  kuishiwa nguvu wakati alipopanda jukwaani  kuwasalimia mashabiki waliofurika kumtizama. 

 Tukio hilo lilitokea Jumapili katika tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika ndani ya uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid wakati msanii huyo alipopandishwa jukwaani kuwasalimia mashabiki wake.

 Mara baada ya msanii huyo kupandishwa jukwaani alipewa kipaza sauti ili aweze kuwasalimia mashabiki wake lakini katika hali ya kawaida alifanikiwa kutamka neno moja tu”ahhh" na kisha kudondoka chini ya jukwaa lakini kabla ya kutua chini alidakwa na wasanii waliokuwa pembeni yake. 

Wasanii wenzie walimkalisha chini ya jukwaa hilo ili aweze kupumzika na kisha baada ya muda mfupi walimshusha chini ya jukwaaa hilo ili aweze kupata muda wa kupumzika zaidi. 

 Akihojiwa  muda mfupi mara baada ya kushuka jukwaani Sajuki kwa sauti ya upole alisema kwamba hali yake kiafya si nzuri kwa kuwa hana nguvu na anahitaji matibabu zaidi. ”Kaka hali yangu si nzuri kabisa naumwa sana sijisikii vizuri”alisema Sajuki huku akionekana mnyonge zaidi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa